Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Zaburi 11:7 - Swahili Revised Union Version

7 Kwa kuwa BWANA ni mwenye haki, Apenda matendo ya haki, Wanyofu wa moyo watauona uso wake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

7 Mwenyezi-Mungu ni mwadilifu na apenda uadilifu; watu wanyofu watakaa pamoja naye.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

7 Mwenyezi-Mungu ni mwadilifu na apenda uadilifu; watu wanyofu watakaa pamoja naye.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

7 Mwenyezi-Mungu ni mwadilifu na apenda uadilifu; watu wanyofu watakaa pamoja naye.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

7 Kwa kuwa Mwenyezi Mungu ni mwenye haki, yeye hupenda haki. Wanyofu watauona uso wake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

7 Kwa kuwa bwana ni mwenye haki, yeye hupenda haki. Wanyofu watauona uso wake.

Tazama sura Nakili




Zaburi 11:7
20 Marejeleo ya Msalaba  

Yeye hawaondolei macho yake wenye haki; Lakini pamoja na wafalme huwaweka Katika viti vya enzi milele, nao hutukuzwa.


BWANA huwafumbua macho waliopofuka; BWANA huwainua walioinama; BWANA huwapenda wenye haki;


Bali mimi nikutazame uso wako katika haki, Niamkapo nishibishwe kwa sura yako.


Maana umemfanya kuwa baraka za milele, Wamfurahisha kwa furaha ya uso wako.


Tazama, jicho la BWANA li kwao wamchao, Wazingojeao fadhili zake.


Huzipenda haki na hukumu, Nchi imejaa fadhili za BWANA.


Macho ya BWANA huwaelekea wenye haki, Na masikio yake hukielekea kilio chao.


Kwa kuwa BWANA hupenda haki, Wala hawaachi watauwa wake. Wao hulindwa milele, Bali mzawa wa wasio haki ataharibiwa.


Nafsi yangu, kwa nini kuinama, Na kufadhaika ndani yangu? Umtumainie Mungu; Kwa maana nitakuja kumsifu, Aliye afya ya uso wangu, Na Mungu wangu.


Umeipenda haki; Umeichukia dhuluma. Kwa hiyo MUNGU, Mungu wako, amekutia mafuta, Mafuta ya furaha kuliko wenzako.


Mavazi yako yote hunukia manemane Na udi na mdalasini. Katika majumba ya pembe Vinubi vimekufurahisha.


Kwa maana Wewe utambariki mwenye haki; BWANA, utamzungushia radhi kama ngao.


Mungu ni mwamuzi mwenye haki, Naam, Mungu akasirikiaye waovu kila siku.


Ubaya wao wasio haki na ukome, Lakini umthibitishe mwenye haki. Kwa maana mjaribu mioyo na fikira Ndiye Mungu aliye mwenye haki.


Mfalme mkuu upendaye hukumu kwa haki; Umeiimarisha haki; Umefanya hukumu na haki katika Israeli.


Njia ya mtu mbaya ni chukizo kwa BWANA; Bali humpenda mtu afuatiaye wema.


Maana mimi, BWANA, naipenda hukumu ya haki, nauchukia wizi na uovu; nami nitawalipa malipo katika kweli, nitaagana nao agano la milele.


Kwa kuwa macho ya Bwana huwaelekea wenye haki, Na masikio yake husikiliza maombi yao; Bali uso wa Bwana uko juu ya watenda mabaya.


Wapenzi, sasa tu wana wa Mungu, wala haijadhihirika bado tutakavyokuwa; lakini tunajua ya kuwa atakapodhihirishwa, tutafanana naye; kwa maana tutamwona kama alivyo.


nao watamwona uso wake, na jina lake litakuwa katika vipaji vya nyuso zao.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo