Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yoshua 3:3 - Swahili Revised Union Version

3 wakawaamuru watu wote wakisema, Mtakapoliona sanduku la Agano la BWANA, Mungu wenu, na makuhani Walawi wakilichukua, ndipo mtakapoondoka hapa mlipo na kulifuata.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 wakawaambia watu, “Mtakapoliona sanduku la agano la Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, limebebwa na makuhani Walawi, mtaondoka na kulifuata;

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

3 wakawaambia watu, “Mtakapoliona sanduku la agano la Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, limebebwa na makuhani Walawi, mtaondoka na kulifuata;

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 wakawaambia watu, “Mtakapoliona sanduku la agano la Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, limebebwa na makuhani Walawi, mtaondoka na kulifuata;

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 wakitoa maagizo kwa watu, wakiwaambia: “Mtakapoona Sanduku la Agano la Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, likichukuliwa na Walawi ambao ndio makuhani, mtaondoka hapo mlipo na kulifuata.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

3 wakitoa maagizo kwa watu, wakiwaambia: “Mtakapoona Sanduku la Agano la bwana Mwenyezi Mungu wenu, likichukuliwa na Walawi ambao ndio makuhani, mtaondoka hapo mlipo na kulifuata.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

3 wakawaamuru watu wote wakisema, Mtakapoliona sanduku la Agano la BWANA, Mungu wenu, na makuhani Walawi wakilichukua, ndipo mtakapoondoka hapa mlipo na kulifuata.

Tazama sura Nakili




Yoshua 3:3
20 Marejeleo ya Msalaba  

Hata ikawa, watu waliolichukua sanduku la BWANA walipokwisha kwenda hatua sita, akachinja fahali na ndama mnono.


Wakaliweka sanduku la Mungu juu ya gari jipya, wakalitoa katika nyumba ya Abinadabu, iliyoko kilimani; nao Uza na Ahio wana wa Abinadabu wakaliendesha lile gari jipya.


Wazee wote wa Israeli wakaja, nao makuhani wakajitwika sanduku.


wala makuhani Walawi hawatakosa kuwa na mtu wa kusimama mbele zangu, na kutoa sadaka za kuteketezwa, na kufukiza matoleo, na kufanya dhabihu daima.


Basi wakasafiri kutoka penye mlima wa BWANA safari ya siku tatu; na sanduku la Agano la BWANA likatangulia mbele yao mwendo wa siku tatu, ili kuwatafutia mahali pa kupumzika.


Na Haruni na wanawe watakapokwisha kupafunika mahali patakatifu, na vyombo vyote vya mahali patakatifu, hapo watakapong'oa kambi; baadaye, wana wa Kohathi watakuja kuvichukua; lakini wasiviguse vile vitu vitakatifu, wasife. Vyombo vile ni mzigo wa wana wa Kohathi katika hema ya kukutania.


Wakati huo Yesu aliwaambia wanafunzi wake, Mtu yeyote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate.


Mwandishi mmoja akamwendea, akamwambia, Mwalimu, nitakufuata kokote uendako.


ndipo Musa akawaamuru Walawi waliokuwa wakilichukua sanduku la Agano la BWANA akawaambia,


Musa akaiandika torati hii, akawapa makuhani, wana wa Lawi, waliolichukua sanduku la Agano la BWANA, na wazee wote wa Israeli.


Lakini, na iwe nafasi kati ya ninyi na lile sanduku, kama dhiraa elfu mbili kiasi chake; msilikaribie mpate kuijua njia ambayo hamna budi kuiendea; kwa maana hamjapita njia hii bado.


Kisha Yoshua akawaambia makuhani, akasema, Liinueni sanduku la Agano, mkavuke mbele ya hao watu. Wakaliinua sanduku la Agano, wakatangulia mbele ya watu.


Nawe uwaamuru hao makuhani walichukuao sanduku la Agano, ukawaambie, Mtakapofika ukingo wa maji ya Yordani, simameni katika Yordani.


Kwa kuwa makuhani waliolichukua hilo sanduku walisimama katikati ya Yordani, hadi mambo yote BWANA aliyomwamuru Yoshua awambie hao watu yakaisha, sawasawa na hayo yote Musa aliyokuwa amemwamuru Yoshua; kisha hao watu wakafanya haraka wakavuka.


Bali Yoshua, mwana wa Nuni, akawaita makuhani, akawaambia, Lichukueni sanduku la Agano, tena makuhani saba na wachukue mabaragumu saba za pembe za kondoo dume watangulie mbele ya sanduku la BWANA.


Hawa ndio wasiojitia unajisi na wanawake, kwa maana ni bikira. Hawa ndio wamfuatao Mwana-kondoo kila aendako. Hawa wamenunuliwa katika wanadamu, malimbuko kwa Mungu na kwa Mwana-kondoo.


Nao Walawi walilishusha sanduku la BWANA, na lile kasha lililokuwa pamoja nalo, lenye vile vitu vya dhahabu; wakaviweka juu ya lile jiwe kubwa; nao watu wa Beth-shemeshi wakatoa sadaka za kuteketezwa, na kuchinja dhabihu siku iyo hiyo kwa BWANA.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo