Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yoshua 24:33 - Swahili Revised Union Version

33 Huyo Eleazari mwana wa Haruni naye akafa; wakamzika Gibea, mji wa Finehasi mwanawe, ambao alipewa katika nchi ya vilima ya Efraimu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

33 Naye Eleazari, mwana wa Aroni, akafariki na kuzikwa Gibea, mji ambao alikuwa amepewa mwanawe Finehasi katika nchi ya milima ya Efraimu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

33 Naye Eleazari, mwana wa Aroni, akafariki na kuzikwa Gibea, mji ambao alikuwa amepewa mwanawe Finehasi katika nchi ya milima ya Efraimu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

33 Naye Eleazari, mwana wa Aroni, akafariki na kuzikwa Gibea, mji ambao alikuwa amepewa mwanawe Finehasi katika nchi ya milima ya Efraimu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

33 Naye Eleazari mwana wa Haruni akafariki, akazikwa huko Gibea, mlima aliokuwa amepewa mtoto wake Finehasi, kwenye nchi ya vilima ya Efraimu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

33 Naye Eleazari mwana wa Haruni akafariki akazikwa huko Gibea, mlima aliokuwa amepewa mtoto wake Finehasi, kwenye nchi ya vilima ya Efraimu.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

33 Huyo Eleazari mwana wa Haruni naye akafa; wakamzika Gibea, mji wa Finehasi mwanawe, ambao alipewa katika nchi ya vilima ya Efraimu.

Tazama sura Nakili




Yoshua 24:33
22 Marejeleo ya Msalaba  

Neno hili silo hivyo; lakini mtu mmoja wa milima ya Efraimu, jina lake, Sheba, mwana wa Bikri, ameinua mkono wake juu ya mfalme, naam, Daudi, basi mtoeni yeye tu, nami nitaondoka katika mji huu. Basi yule mwanamke akamwambia Yoabu, Tazama, kichwa chake utatupiwa juu ya ukuta.


Na haya ndiyo majina yao. Mwana wa Huri, mlimani mwa Efraimu.


Akasema, Amani. Bwana wangu amenituma, kusema, Tazama, sasa hivi wamenijia kutoka milimani mwa Efraimu vijana wawili wa wana na manabii; uwape, nakuomba, talanta ya fedha, na mavazi mawili.


mwana wa Abishua, mwana wa Finehasi, mwana wa Eleazari, mwana wa Haruni, kuhani mkuu;


Kwani najua kuwa utanileta hata kifoni, Niifikie nyumba waliyoaandaliwa wenye uhai wote.


Naam, ataliona, hata wenye hekima hufa; Mpumbavu na mjinga hupotea pamoja, Na kuwaachia wengine mali zao.


Haruni akamwoa Elisheba, binti ya Aminadabu, dada yake Nashoni; naye akamzalia Nadabu, na Abihu, na Eleazari, na Ithamari.


Na Eleazari mwana wa Haruni akamwoa mmoja miongoni mwa binti za Putieli; naye akamzalia Finehasi. Hawa ndio vichwa vya nyumba za baba wa Walawi kulingana na jamaa zao.


Je, Baba zenu wako wapi? Je, manabii nao wanaishi milele?


Na Eleazari mwana wa Haruni kuhani atakuwa mkuu wa hao wakuu wa Walawi, naye atawasimamia hao wahudumu wa mahali patakatifu.


Kwa maana Daudi, akiisha kulitumikia shauri la Mungu katika kizazi chake, alilala, akawekwa pamoja na baba zake, akaona uharibifu.


bali yeye, kwa kuwa anakaa milele, anao ukuhani wake usioondoka.


Kisha hizi ndizo nchi ambazo wana wa Israeli walizitwaa katika nchi ya Kanaani, ambazo Eleazari kuhani, na Yoshua mwana wa Nuni, na vichwa vya nyumba za mababa wa makabila ya Israeli, waliwagawanyia,


Kisha wana wa Israeli wakatuma wajumbe waende kwa wana wa Reubeni, na wana wa Gadi, na hiyo nusu ya kabila la Manase, hadi nchi ya Gileadi; nao ni hawa, Finehasi mwana wa Eleazari kuhani;


Mtu huyo akatoka katika huo mji, Bethlehemu-yuda, ili aende kukaa kama mgeni hapo atakapoona mahali; akafikia nchi ya vilima vilima ya Efraimu katika safari yake, hadi nyumba ya huyo Mika.


Nao wakapita huko hadi hiyo nchi ya vilima vilima ya Efraimu, wakafikia nyumba ya huyo Mika.


na Finehasi, mwana wa Eleazari, mwana wa Haruni, alikuwa anasimama mbele ya hilo sanduku siku hizo), wakasema, Je! Nitoke tena niende kupigana na wana wa Benyamini ndugu yangu, au niache? BWANA akawaambia, Haya, kweeni; kwa kuwa kesho nitamtoa na kumtia mkononi mwako.


Palikuwa na mtu mmoja wa Rama, Msufi, wa nchi ya milima milima ya Efraimu, jina lake akiitwa Elkana, mwana wa Yerohamu, mwana wa Elihu, mwana wa Tohu, mwana wa Sufu, Mwefraimu


Naye akapita katika nchi ya milima milima ya Efraimu, akapita katika nchi ya Shalisha, lakini hawakuwaona; kisha wakapita katika nchi ya Shaalimu, wala huko hawakuwako; wakapita katika nchi ya Wabenyamini, lakini hawakuwapata.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo