Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Yoshua 20:4 - Swahili Revised Union Version

4 Naye ataikimbilia miji hiyo mmojawapo, naye atasimama hapo penye maingilio ya lango la huo mji, kisha atanena neno lake masikioni mwa wazee wa mji; nao watamtia kwao ndani ya mji, na kumpa mahali, ili apate kukaa kati yao.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 Mwuaji atakimbilia katika mji mmojawapo na kusimama mlangoni mwa mji na kuwaeleza wazee wa mji huo kesi yake. Wazee watampokea ndani na kumpa mahali pa kuishi pamoja nao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 Mwuaji atakimbilia katika mji mmojawapo na kusimama mlangoni mwa mji na kuwaeleza wazee wa mji huo kesi yake. Wazee watampokea ndani na kumpa mahali pa kuishi pamoja nao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 Mwuaji atakimbilia katika mji mmojawapo na kusimama mlangoni mwa mji na kuwaeleza wazee wa mji huo kesi yake. Wazee watampokea ndani na kumpa mahali pa kuishi pamoja nao.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 “Anapokimbilia mojawapo ya hii miji, atasimama kwenye maingilio ya lango la mji mkuu na kueleza wazee wa mji kuhusu shauri lake. Kisha watampokea katika mji wao na kumpa mahali pa kuishi nao.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 “Anapokimbilia mojawapo ya hii miji mikubwa atasimama kwenye maingilio ya lango la mji mkuu na kueleza wazee wa mji kuhusu shauri lake. Kisha watampokea katika mji wao na kumpa mahali pa kuishi nao.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

4 Naye ataikimbilia miji hiyo mmojawapo, naye atasimama hapo penye maingilio ya lango la huo mji, kisha atanena neno lake masikioni mwa wazee wa mji; nao watamtia kwao ndani ya mji, na kumpa mahali, ili apate kukaa kati yao.

Tazama sura Nakili

Yoshua 20:4
8 Marejeleo ya Msalaba  

Wakati nilipotoka kwenda mjini, kupitia langoni, Nilipokitengeza kiti changu katika njia kuu,

Watoto wake wako mbali na wokovu, Nao wamesongwa langoni, Wala hapana atakayewaponya.

Usiiondoe nafsi yangu pamoja na wakosaji, Wala uhai wangu pamoja na wauaji.

Mume wake hujulikana malangoni; Aketipo pamoja na wazee wa nchi.

Basi, Ebedmeleki, Mkushi, towashi, aliyekuwa katika nyumba ya mfalme, aliposikia kwamba wamemtia Yeremia shimoni; na wakati huo mfalme alikuwa amekaa katika lango la Benyamini;

ili kwa vitu viwili visivyoweza kubadilika, ambavyo katika hivyo Mungu hawezi kusema uongo, tupate faraja iliyo imara, sisi tuliokimbilia kuyashika matumaini yale yawekwayo mbele yetu;

ili kwamba mwenye kuua mtu, aliyemwua mtu yeyote pasipo kukusudia, na pasipo kujua, apate kukimbilia huko; nayo itakuwa ni mahali pa kukimbilia kwenu, kumkimbia huyo ajilipizaye kisasi cha damu.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo