Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yoshua 10:12 - Swahili Revised Union Version

12 Ndipo Yoshua akanena na BWANA katika siku hiyo ambayo BWANA aliwatoa Waamori mbele ya wana wa Israeli; akasema mbele ya macho ya Israeli, Wewe Jua, simama kimya juu ya Gibeoni; Na wewe Mwezi, simama katika bonde la Aiyaloni.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

12 Wakati Mwenyezi-Mungu alipowatia Waamori mikononi mwa Waisraeli, Yoshua alimwomba Mwenyezi-Mungu mbele ya Waisraeli wote, akasema, “Wewe jua, simama kimya juu ya Gibeoni, wewe mwezi, katika bonde la Aiyaloni.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

12 Wakati Mwenyezi-Mungu alipowatia Waamori mikononi mwa Waisraeli, Yoshua alimwomba Mwenyezi-Mungu mbele ya Waisraeli wote, akasema, “Wewe jua, simama kimya juu ya Gibeoni, wewe mwezi, katika bonde la Aiyaloni.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

12 Wakati Mwenyezi-Mungu alipowatia Waamori mikononi mwa Waisraeli, Yoshua alimwomba Mwenyezi-Mungu mbele ya Waisraeli wote, akasema, “Wewe jua, simama kimya juu ya Gibeoni, wewe mwezi, katika bonde la Aiyaloni.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

12 Siku ile Mwenyezi Mungu alipowakabidhi Waamori kwa Waisraeli, Yoshua akanena na Mwenyezi Mungu akiwa mbele ya Waisraeli, akasema: “Wewe jua, simama juu ya Gibeoni, wewe mwezi, tulia juu ya Bonde la Aiyaloni.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

12 Katika siku ile ambayo bwana aliwapeana Waamori kwa Israeli, Yoshua akanena na bwana akiwa mbele ya Waisraeli akasema: “Wewe jua, simama juu ya Gibeoni, wewe mwezi, tulia juu ya Bonde la Aiyaloni.”

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

12 Ndipo Yoshua akanena na BWANA katika siku hiyo ambayo BWANA aliwatoa Waamori mbele ya wana wa Israeli; akasema mbele ya macho ya Israeli, Wewe Jua, simama kimya juu ya Gibeoni; Na wewe Mwezi, simama katika bonde la Aiyaloni.

Tazama sura Nakili




Yoshua 10:12
29 Marejeleo ya Msalaba  

Basi Abneri, mwana wa Neri, na watumishi wa Ishboshethi, mwana wa Sauli, wakatoka Mahanaimu kwenda Gibeoni.


Hezekia akajibu, Ni jambo jepesi kivuli kuendelea madaraja kumi; la, hicho kivuli na kirudi nyuma madaraja kumi.


Isaya nabii akamlilia BWANA; akakirudisha nyuma kile kivuli madaraja kumi, ambayo kilikuwa kimeshuka katika madaraja ya Ahazi.


Isaya akamwambia, Jambo hili litakuwa ishara kwako, itokayo kwa BWANA, ya kwamba BWANA atalifanya neno hilo alilolinena; je! Kivuli kiendelee madaraja kumi, au kirudi nyuma madaraja kumi?


na Beria, na Shema, waliokuwa wakuu wa mbari za baba zao miongoni mwa wenyeji wa Aiyaloni, wale ambao waliwakimbiza wenyeji wa Gathi.


Sora, Aiyaloni, na Hebroni, iliyoko katika Yuda na Benyamini, miji yenye maboma.


Aliamuruye jua, nalo halichomozi; Nazo nyota huzipiga mhuri.


Msifuni, jua na mwezi; Msifuni, nyota zote zenye mwanga.


Sauti yao imeenea duniani kote, Na maneno yao hadi miisho ya ulimwengu. Katika hizo ameliwekea jua hema,


Mchana ni wako, usiku nao ni wako, Ndiwe uliyeufanya mwanga na jua.


Maana BWANA ataondoka kama vile katika mlima Perasimu, ataghadhibika kama vile katika bonde la Gibeoni; apate kufanya kazi yake, kazi yake ya ajabu; na kulitimiza tendo lake, tendo lake la ajabu.


Tazama, nitakirudisha nyuma kivuli madaraja kumi, ambayo kilishuka juu ya duara ya Ahazi kwa sababu ya jua. Basi jua likarudi madaraja kumi katika hiyo duara, ambayo limekwisha kushuka.


Jua lako halitashuka tena, Wala mwezi wako hautajitenga; Kwa kuwa BWANA mwenyewe atakuwa nuru yako ya milele; Na siku za kuomboleza kwako zitakoma.


Ikawa, katika mwaka ule ule, mwanzo wa kutawala kwake Sedekia, mfalme wa Yuda, mwaka wa nne, mwezi wa tano, Hanania, mwana wa Azuri, nabii, wa Gibeoni, akasema nami ndani ya nyumba ya BWANA, mbele ya makuhani na watu wote, akisema,


Lakini nilimwangamiza Mwamori mbele yao, ambaye urefu wake ulikuwa kama urefu wa mierezi, tena alikuwa na nguvu kama mialoni; lakini niliyaangamiza matunda yake toka juu, na mizizi yake toka chini.


Tena itakuwa siku hiyo, asema Bwana MUNGU, nitalifanya jua litue wakati wa adhuhuri, nami nitaitia nchi giza wakati wa nuru ya mchana.


Lakini BWANA yumo ndani ya hekalu lake takatifu; dunia yote na inyamaze kimya mbele zake.


Jua na mwezi vikasimama makaoni mwao; Mbele ya nuru ya mishale yako ilipotapakaa, Mbele ya mwangaza wa mkuki wako umeremetao.


Nyamazeni, ninyi nyote wenye mwili, mbele za BWANA; kwa maana ameamka, na kutoka katika maskani yake takatifu.


naye amekwenda kutumikia miungu mingine na kuiabudu, au jua, au mwezi, au vilivyo katika jeshi la mbinguni vyovyote, nisivyoagiza mimi;


tena usije ukainua macho yako hata mbinguni, na ulionapo jua, na mwezi, na nyota, jeshi la mbinguni lote pia, ukashawishwa na kuviabudu, na kuvitumikia, ambavyo BWANA, Mungu wako amewagawanyia watu wote chini ya mbingu zote.


Ndipo jua likasimama, na mwezi ukatulia, Hadi hilo taifa lilipokuwa limekwisha jilipiza kisasi juu ya adui zao. Hayo, je! Hayakuandikwa ndani ya kitabu cha Yashari? Basi jua likasimama kimya katikati ya mbingu, wala halikufanya haraka kuchwa kama muda wa siku nzima.


Shaalabini, Aiyaloni, Ithla;


na Aiyaloni pamoja na mbuga zake za malisho, na Gath-rimoni pamoja na mbuga zake za malisho; miji minne.


Huyo Eloni, Mzabuloni, akafa, akazikwa katika Aiyaloni katika nchi ya Zabuloni.


Walipigana kutoka mbinguni, Nyota katika miendo yao zilipigana na Sisera.


Basi Samweli akamwomba BWANA, naye BWANA akatuma ngurumo na mvua siku ile; nao watu wote wakamwogopa BWANA sana, na Samweli pia.


Nao wakawapiga watu miongoni mwa Wafilisti siku ile kutoka Mikmashi mpaka Ayaloni; na hao watu walikuwa wamepungukiwa sana na nguvu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo