Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yoshua 1:17 - Swahili Revised Union Version

17 Kama vile tulivyomsikiliza Musa katika mambo yote, ndivyo tutakavyokusikiliza wewe; BWANA, Mungu wako, na awe pamoja nawe tu, kama alivyokuwa pamoja na Musa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

17 Kama vile tulivyomtii Mose katika mambo yote, ndivyo tutakavyokutii wewe; Mwenyezi-Mungu, Mungu wako na awe pamoja nawe kama alivyokuwa pamoja na Mose.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

17 Kama vile tulivyomtii Mose katika mambo yote, ndivyo tutakavyokutii wewe; Mwenyezi-Mungu, Mungu wako na awe pamoja nawe kama alivyokuwa pamoja na Mose.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

17 Kama vile tulivyomtii Mose katika mambo yote, ndivyo tutakavyokutii wewe; Mwenyezi-Mungu, Mungu wako na awe pamoja nawe kama alivyokuwa pamoja na Mose.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

17 Kama vile tulivyomtii Musa kikamilifu, ndivyo tutakavyokutii wewe. Mwenyezi Mungu, Mungu wako, na awe pamoja nawe tu kama vile alivyokuwa pamoja na Musa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

17 Kama vile tulivyomtii Musa kikamilifu, ndivyo tutakavyokutii wewe. bwana Mwenyezi Mungu wako na awe pamoja nawe tu kama vile alivyokuwa pamoja na Musa.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

17 Kama vile tulivyomsikiliza Musa katika mambo yote, ndivyo tutakavyokusikiliza wewe; BWANA, Mungu wako, na awe pamoja nawe tu, kama alivyokuwa pamoja na Musa.

Tazama sura Nakili




Yoshua 1:17
19 Marejeleo ya Msalaba  

Ndipo mimi mjakazi wako nikasema, Neno la bwana wangu mfalme na liwe la kustarehesha; kwa kuwa kama malaika wa Mungu ndivyo alivyo bwana wangu mfalme, kuyapambanua yaliyo mema na yaliyo mabaya; naye BWANA, Mungu wako na awe pamoja nawe.


Kama vile BWANA alivyokuwa pamoja na bwana wangu mfalme, kadhalika na awe pamoja na Sulemani, na kufanya kiti chake cha enzi kuwa kitukufu kuliko kiti cha enzi cha bwana wangu mfalme Daudi.


Kisha Daudi akamwambia Sulemani mwanawe, Uwe hodari, mwenye moyo mkuu, ukatende hivyo; usiogope wala usifadhaike; kwa kuwa BWANA, Mungu, Mungu wangu, yu pamoja nawe; yeye hatakupungukia wala kukuacha, hata itakapomalizika kazi yote ya huo utumishi wa nyumba ya BWANA.


BWANA akujibu siku ya dhiki, Jina la Mungu wa Yakobo likuinue.


Akujalie kwa kadiri ya haja ya moyo wako, Na kukutimizia mipango yako yote.


BWANA, umwokoe mfalme, Utuitikie siku tuitayo.


BWANA akamwambia Musa, Mtwae Yoshua, mwana wa Nuni, mtu ambaye roho iko ndani yake, ukamwekee mkono wako;


Nawe utaweka juu yake sehemu ya heshima yako, ili jumuiya yote ya wana wa Israeli wapate kutii.


Na makutano waliotangulia, na wale waliofuata, wakapaza sauti, wakisema, Hosana, Mwana wa Daudi; ndiye mbarikiwa, yeye ajaye kwa jina la Bwana; Hosana juu mbinguni.


Na Yoshua, mwana wa Nuni, alikuwa amejaa roho ya hekima; maana Musa alikuwa amemwekea mikono yake juu yake; wana wa Israeli wakamsikiliza, wakafanya kama BWANA alivyomwamuru Musa.


Wakamjibu Yoshua, wakasema, Hayo yote uliyotuamuru tutayafanya, na kila mahali utakakotutuma tutakwenda.


Kila mtu atakayeiasi amri yako, asiyasikilize maneno yako katika mambo yote utakayomwamuru, atauawa. Uwe hodari na moyo wa ushujaa, hilo tu.


Hakuna mtu yeyote atakayeweza kusimama mbele yako siku zote za maisha yako; kama nilivyokuwa pamoja na Musa, ndivyo nitakavyokuwa pamoja na wewe; sitakupungukia wala sitakuacha.


Je! Si mimi niliyekuamuru? Uwe hodari na moyo wa ushujaa; usiogope wala usifadhaike; kwa kuwa BWANA, Mungu wako, yu pamoja nawe kila uendako.


Siku ile BWANA alimtukuza Yoshua mbele ya macho ya Israeli wote; nao wakamcha, kama walivyokuwa wakimcha Musa, siku zote za maisha yake.


Daudi akasema, BWANA aliyeniokoa na makucha ya simba, na makucha ya dubu, ataniokoa na mkono wa Mfilisti huyu. Sauli akamwambia Daudi, Nenda, na BWANA atakuwa pamoja nawe.


BWANA anitende mimi, Yonathani, hivyo, na kuzidi, ikiwa yampendeza babangu kukutenda mabaya, nisipokufunulia haya, na kukutuma uende zako kwa amani; na BWANA awe pamoja nawe, kama alivyokuwa pamoja na baba yangu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo