Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yohana 21:19 - Swahili Revised Union Version

19 Akasema neno hilo kwa kuonesha ni kwa mauti gani atakayomtukuza Mungu. Naye akiisha kusema hayo akamwambia, Nifuate.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

19 (Kwa kusema hivyo, alionesha jinsi Petro atakavyokufa na kumtukuza Mungu). Kisha akamwambia, “Nifuate.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

19 (Kwa kusema hivyo, alionesha jinsi Petro atakavyokufa na kumtukuza Mungu). Kisha akamwambia, “Nifuate.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

19 (Kwa kusema hivyo, alionesha jinsi Petro atakavyokufa na kumtukuza Mungu). Kisha akamwambia, “Nifuate.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

19 Isa alisema haya ili kuashiria aina ya kifo ambacho Petro angemtukuza nacho Mungu. Kisha Isa akamwambia Petro, “Nifuate!”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

19 Isa alisema haya ili kuashiria ni kifo cha aina gani Petro atakachomtukuza nacho Mungu. Kisha Isa akamwambia Petro, “Nifuate!”

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

19 Akasema neno hilo kwa kuonesha ni kwa mauti gani atakayomtukuza Mungu. Naye akiisha kusema hayo akamwambia, Nifuate.

Tazama sura Nakili




Yohana 21:19
17 Marejeleo ya Msalaba  

lakini mtumishi wangu Kalebu, kwa kuwa alikuwa na roho nyingine ndani yake, naye amenifuata kwa moyo wote, nitamleta yeye mpaka nchi hiyo aliyoingia; na wazao wake wataimiliki.


Wala mtu asiyechukua msalaba wake akanifuata, hanistahili.


Yesu akawaambia, Amin, nawaambia ya kwamba ninyi mlionifuata mimi, katika ulimwengu mpya, atakapoketi Mwana wa Adamu katika kiti cha utukufu wake, ninyi nanyi mtaketi katika viti kumi na viwili, mkiwahukumu makabila kumi na mawili ya Israeli.


Lakini Yesu akamwambia, Nifuate; waache wafu wazike wafu wao.


Mtu akinitumikia, na anifuate; nami nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo. Tena mtu akinitumikia, Baba atamheshimu.


Aliyanena hayo akionesha ni mauti gani atakayokufa.


Ili litimie lile neno lake Yesu alilolisema, akionesha ni mauti gani atakayokufa.


Akasema, Amin, amin, nakuambia, Wakati ulipokuwa kijana, ulikuwa ukijifunga mwenyewe na kwenda utakako; lakini utakapokuwa mzee, utainyosha mikono yako, na mwingine atakufunga na kukuchukua usikotaka.


Yesu akamwambia, Ikiwa nataka huyu akae hata nitakapokuja, imekuhusuje wewe? Wewe unifuate mimi.


kama vile nilivyotazamia sana, na kutumaini, kwamba sitaaibika kamwe, bali kwa uthabiti wote, kama sikuzote na sasa vivyo hivyo Kristo ataadhimishwa katika mwili wangu; ikiwa kwa maisha yangu, au ikiwa kwa mauti yangu.


Nikijua kwamba kule kuwekea mbali maskani yangu kwaja upesi, kama Bwana wetu Yesu Kristo alivyonionesha.


Samweli akawaambia, Msiogope; ni kweli mmeutenda uovu huu wote; lakini msigeuke na kuacha kumfuata BWANA, bali mtumikieni BWANA kwa mioyo yenu yote.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo