Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 8:16 - Swahili Revised Union Version

16 Kutoka Dani kumesikiwa mkoromo wa farasi wake; nchi yote pia inatetemeka kwa sauti ya mlio wa farasi wake wa vita; maana wamekuja, wamekula nchi na vyote vilivyomo; huo mji na wote wakaao ndani yake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 Sauti za farasi wao zinasikika, kwa mlio wa farasi wao wa vita, nchi nzima inatetemeka. Wanafika na kuiharibu nchi na vyote vilivyomo, kuangamiza mji pamoja na wote waishio humo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 Sauti za farasi wao zinasikika, kwa mlio wa farasi wao wa vita, nchi nzima inatetemeka. Wanafika na kuiharibu nchi na vyote vilivyomo, kuangamiza mji pamoja na wote waishio humo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 Sauti za farasi wao zinasikika, kwa mlio wa farasi wao wa vita, nchi nzima inatetemeka. Wanafika na kuiharibu nchi na vyote vilivyomo, kuangamiza mji pamoja na wote waishio humo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 Mkoromo wa farasi wa adui umesikika kuanzia Dani, kwa mlio wa madume yao ya farasi, nchi yote inatetemeka. Wamekuja kuangamiza nchi na vyote vilivyomo, mji na wote wanaoishi ndani yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 Mkoromo wa farasi za adui umesikika kuanzia Dani, kwa mlio wa madume yao ya farasi, nchi yote inatetemeka. Wamekuja kuangamiza nchi na vyote vilivyomo, mji na wote waishio ndani yake.”

Tazama sura Nakili




Yeremia 8:16
22 Marejeleo ya Msalaba  

Ndiwe uliyemfanya aruke kama nzige? Fahari ya mlio wake hutisha.


Nchi na vyote vilivyomo ni mali ya BWANA, Dunia na wote wakaao ndani yake.


Hasira yako uwamwagie mataifa wasiokujua, na jamaa zao wasioliitia jina lako; kwa maana wamemla Yakobo, naam, wamemla kabisa na kumwangamiza, na kuyafanya makao yake kuwa ukiwa.


Lakini kitu cha aibu kimeila kazi ya baba zetu tokea ujana wetu; makundi yao ya kondoo na ng'ombe, wana wao na binti zao.


Basi, watu wote wakulao wataliwa; na adui zako wote watakwenda kufungwa; kila mmoja wao; na hao waliokuteka nyara watatekwa; na wote waliokuwinda nitawafanya kuwa mawindo.


Maana BWANA asema hivi, Tumesikia sauti ya tetemeko, na ya hofu, wala si ya amani.


Niliiangalia milima, na tazama, ilitetemeka, na milima yote ilisogea huku na huko.


Simba ametoka katika kichaka chake, ndiye aangamizaye mataifa; ameanza kushika njia, ametoka katika mahali pake; ili aifanye nchi yako kuwa ukiwa, miji yako ifanywe maganjo, asibaki mwenyeji ndani yake.


Kwa sababu ya kishindo cha kukanyaga kwa kwato za farasi wake walio hodari, kwa sababu ya mwendo wa mbio mbio wa magari yake ya vita; kwa sababu ya mngurumo wa magurudumu yake, hao akina baba hawatazami nyuma ili kuwaangalia watoto wao, kwa kuwa mikono yao ni dhaifu;


Nao watakula mavuno yako, na mkate wako, ambao iliwapasa wana wako na binti zako kuula; watakula makundi yako ya kondoo na ya ng'ombe; watakula mizabibu yako na mitini yako; wataiharibu miji yako yenye boma, uliyokuwa ukiitumainia, naam, wataiharibu kwa upanga.


Wanashika upinde na mkuki; Ni wakatili, hawana huruma; Sauti yao inanguruma kama bahari, Nao wamepanda farasi; Kila mmoja amejipanga kama aendaye vitani, Juu yako, Ee binti Babeli.


Nayo nchi yatetemeka, nayo ina uchungu; maana makusudi ya BWANA juu ya Babeli yasimama, kuifanya nchi ya Babeli ukiwa, isikaliwe na mtu.


Washika upinde na mkuki; ni wakatili, hawana huruma; sauti yao huvuma kama bahari, nao wamepanda farasi wao; kila mmoja kama mtu wa vita amejipanga juu yako, Ee binti Sayuni.


Kelele za mjeledi, kelele za magurudumu yafanyayo kishindo; na farasi wenye kuparapara, na magari ya vita yenye kurukaruka;


Milima ilikuona, ikaogopa; Gharika ya maji ikapita; Vilindi vikatoa sauti yake, Vikainua juu mikono yake.


maana, Dunia ni mali ya Bwana na vyote viijazavyo.


Lakini mtu akiwaambia, Kitu hiki kimetolewa kiwe sadaka, msile, kwa ajili yake yeye aliyewaambia, na kwa ajili ya dhamiri.


Wakauita mji jina lake Dani, kwa kulifuata jina la baba yao Dani, aliyezaliwa na Israeli; lakini jina la mji huo hapo awali lilikuwa Laisha.


Ndipo wana wa Israeli walipotoka; na mkutano ukakutanika kama mtu mmoja, kutoka Dani hadi Beer-sheba, pamoja na nchi ya Gileadi wakamkutanikia BWANA huko Mispa.


Kisha, kwa kishindo kwato za farasi zilipigapiga, Kwa maana walivyoenda shoti, Walipowakimbiza farasi wenye nguvu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo