Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 7:21 - Swahili Revised Union Version

21 BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Tieni sadaka zenu za kuteketezwa pamoja na dhabihu zenu, mkale nyama.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

21 Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi: “Haya, ongezeni tambiko zenu za kuteketezwa juu ya sadaka zenu na kula nyama yake!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

21 Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi: “Haya, ongezeni tambiko zenu za kuteketezwa juu ya sadaka zenu na kula nyama yake!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

21 Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi: “Haya, ongezeni tambiko zenu za kuteketezwa juu ya sadaka zenu na kula nyama yake!

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

21 “ ‘Hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, Mungu wa Israeli: Endeleeni, ongezeni sadaka zenu za kuteketezwa juu ya dhabihu zenu nyingine, mle nyama hiyo wenyewe!

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

21 “ ‘Hivi ndivyo asemavyo bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli: Endeleeni, ongezeni sadaka zenu za kuteketezwa juu ya dhabihu zenu nyingine, mle nyama hiyo wenyewe!

Tazama sura Nakili




Yeremia 7:21
9 Marejeleo ya Msalaba  

Sitakukemea kwa ajili ya dhabihu zako, Na kafara zako ziko mbele zangu daima.


Hukuniletea wana-kondoo kuwa kafara zako, wala hukuniheshimu kwa dhabihu zako. Sikukutumikisha kwa matoleo, wala sikukuchosha kwa ubani.


Wafungapo, mimi sitasikia kilio chao; na watoapo sadaka za kuteketezwa na sadaka ya unga, sitazitakabali; bali nitawaangamiza kwa upanga, na kwa njaa, na kwa tauni.


Yafaa nini niletewe ubani kutoka Sheba, na udi kutoka nchi iliyo mbali? Sadaka zenu za kuteketezwa hazikubaliwi, wala dhabihu zenu haziniridhii.


Basi, waambie, Bwana MUNGU asema hivi; Mnakula nyama pamoja na damu yake, na kuviinulia vinyago vyenu macho yenu, na kumwaga damu; je, mtaimiliki nchi hii?


Kwa habari za dhabihu za matoleo yangu, hutoa dhabihu ya nyama na kuila; lakini BWANA hawakubali; sasa ataukumbuka uovu wao, na kuwapatiliza dhambi zao; watarudi kwenda Misri.


nawe zisongeze sadaka zako za kuteketezwa, nyama na damu, juu ya madhabahu ya BWANA, Mungu wako; na damu ya dhabihu zako uimwage juu ya madhabahu ya BWANA, Mungu wako, na wewe utakula nyama yake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo