Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 6:5 - Swahili Revised Union Version

5 Inukeni, na tupande juu wakati wa usiku, tukayaharibu majumba yake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 Basi, tutaushambulia usiku; tutayaharibu majumba yake ya kifalme.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

5 Basi, tutaushambulia usiku; tutayaharibu majumba yake ya kifalme.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 Basi, tutaushambulia usiku; tutayaharibu majumba yake ya kifalme.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 Kwa hiyo inukeni, tufanye mashambulizi usiku, na kuharibu ngome zake!”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 Kwa hiyo inukeni, tufanye mashambulizi usiku, na kuharibu ngome zake!”

Tazama sura Nakili




Yeremia 6:5
12 Marejeleo ya Msalaba  

Wakaiteketeza nyumba ya Mungu, wakaubomoa ukuta wa Yerusalemu, wakayateketeza kwa moto majumba yake yote, wakaviharibu vyombo vyake vyote vya thamani.


Mungu katika majumba yake Amejijulisha kuwa ngome.


maana jumba la mfalme litaachwa; mji uliokuwa na watu wengi utakuwa hauna mtu; kilima na mnara utakuwa makao ya wanyama milele, furaha ya punda mwitu, malisho ya makundi ya kondoo;


Lakini kama hamtaki kunisikiliza, kuitakasa siku ya sabato, kutokuchukua mzigo katika malango ya Yerusalemu siku ya sabato; basi, nitawasha moto malangoni mwake, nao utaziteketeza nyumba za enzi za Yerusalemu, wala hautazimika.


Akaiteketeza nyumba ya BWANA, na nyumba ya mfalme; na nyumba zote za Yerusalemu, naam, kila nyumba kubwa aliiteketeza kwa moto.


Ukuta wa mji ukabomolewa, watu wote wa vita wakakimbia, wakatoka mjini usiku, kwa njia ya lango lililokuwa kati ya zile kuta mbili, karibu na bustani ya mfalme; (basi wale Wakaldayo walikuwa wameuzunguka mji pande zote;) wakaenda zao kwa njia ya Araba.


Kwa maana mauti imepandia madirishani mwetu, imeingia majumbani mwetu; Ipate kuwakatilia mbali watoto walio nje, na vijana katika njia kuu.


Maana Israeli amemsahau Muumba wake, naye amejenga nyumba za enzi; na Yuda ameongeza miji yenye maboma; lakini nitatuma moto juu ya miji yake, nao utaziteketeza ngome zake.


lakini nitatuma moto juu ya Yuda, nao utayateketeza majumba ya Yerusalemu. Hukumu kwa Israeli.


Maono yake Obadia. Ndivyo asemavyo Bwana MUNGU juu ya Edomu; Tumepata habari kwa BWANA, Na mjumbe ametumwa kati ya mataifa, Akisema, Haya, inukeni ninyi; Na tuinuke tupigane naye.


Ifungue milango yako, Ee Lebanoni, Ili moto uiteketeze mierezi yako.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo