Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 43:1 - Swahili Revised Union Version

1 Ikawa Yeremia alipokwisha kuwaambia watu wote maneno yote ya BWANA, Mungu wao, ambayo BWANA, Mungu wao, amemtuma kwao, yaani, maneno hayo yote,

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Yeremia alipomaliza kuwaambia watu wote maneno yote ambayo Mwenyezi-Mungu, Mungu wao, alimwamuru awatangazie,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Yeremia alipomaliza kuwaambia watu wote maneno yote ambayo Mwenyezi-Mungu, Mungu wao, alimwamuru awatangazie,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Yeremia alipomaliza kuwaambia watu wote maneno yote ambayo Mwenyezi-Mungu, Mungu wao, alimwamuru awatangazie,

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Yeremia alipomaliza kuwaambia watu maneno yote ya Mwenyezi Mungu, Mungu wao, yaani kila kitu Mwenyezi Mungu alichokuwa amemtuma kuwaambia,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Yeremia alipomaliza kuwaambia watu maneno yote ya bwana Mwenyezi Mungu wao, yaani kila kitu bwana alichokuwa amemtuma kuwaambia,

Tazama sura Nakili




Yeremia 43:1
15 Marejeleo ya Msalaba  

Lutu akatoka na kusema na wachumba wa binti zake, akawaambia, “Ondokeni mahali hapa kwa sababu BWANA atauharibu mji huu”. Lakini akaonekana kama achezaye machoni pa wakwe zake.


Musa akaenda akawaambia watu maneno yote ya BWANA, na hukumu zake zote; watu wote wakajibu kwa sauti moja, wakasema, Maneno yote aliyoyanena BWANA tutayatenda.


Haya basi, wewe jifunge viuno, ukaondoke ukawaambie maneno yote niliyokuamuru; usifadhaike kwa ajili yao, nisije nikakufadhaisha wewe mbele yao.


Lakini BWANA akaniambia, Usiseme, Mimi ni mtoto; maana utakwenda kwa kila mtu nitakayekutuma kwake, nawe utasema kila neno nitakalokuamuru.


BWANA asema hivi, Simama katika uwanja wa nyumba ya BWANA, useme na miji yote ya Yuda, wajao ili kuabudu katika nyumba ya BWANA; sema nao maneno yote ninayokuamuru kuwaambia, usizuie hata neno moja.


Ikawa, Yeremia alipokuwa amekwisha kusema maneno yote BWANA aliyomwamuru kuwaambia watu wote, ndipo hao makuhani, na manabii, na watu wote, wakamkamata, wakisema, Bila shaka utakufa.


nami nimewafunulia haya leo; lakini ninyi hamkuitii sauti ya BWANA, Mungu wenu, katika neno lolote ambalo amenituma kwenu.


Basi, sasa jueni sana ya kuwa mtakufa kwa upanga, na kwa njaa, na kwa tauni, katika mahali pale mnapopatamani kwenda na kukaa.


Wamemkataa BWANA, na kusema, Si yeye; wala hayatatupata mabaya; wala hatutaona upanga wala njaa;


Tena itakuwa utakapokwisha kukisoma kitabu hicho, utakifungia jiwe, na kukitupa katika mto Frati;


na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.


Kwa maana sikujiepusha na kuwahubiria habari ya kusudi lote la Mungu.


Nendeni mkasimame hekaluni mkawaambie watu maneno yote ya Uzima huu.


Naye Samweli akawaambia wale watu waliotaka mfalme maneno yote ya BWANA.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo