Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 4:21 - Swahili Revised Union Version

21 Niione bendera hata lini, na kuisikia sauti ya tarumbeta?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

21 Hadi lini nitaona bendera ya vita na kuisikia sauti ya tarumbeta?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

21 Hadi lini nitaona bendera ya vita na kuisikia sauti ya tarumbeta?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

21 Hadi lini nitaona bendera ya vita na kuisikia sauti ya tarumbeta?

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

21 Hata lini nitaendelea kuona bendera ya vita na kusikia sauti za tarumbeta?

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

21 Hata lini nitaendelea kuona bendera ya vita na kusikia sauti za tarumbeta?

Tazama sura Nakili




Yeremia 4:21
11 Marejeleo ya Msalaba  

Naye Yeremia akamlilia Yosia; na waimbaji wote wanaume kwa wawanawake wakamtaja Yosia katika maombolezo yao, hadi leo; hata wakayafanya kuwa ada kwa Israeli; nayo, tazama, yameandikwa katika Maombolezo.


Mwaka ulipokwisha, Nebukadneza akatuma wajumbe, akamchukua mpaka Babeli; pamoja na vyombo vya thamani vya nyumba ya BWANA; akamtawaza Sedekia nduguye awe mfalme juu ya Yuda na Yerusalemu.


Kwa hiyo akaleta juu yao mfalme wa Wakaldayo, aliyewaua vijana wao kwa upanga nyumbani mwa patakatifu pao, asiwahurumie kijana wala mwanamwali, mzee wala mnyonge; akawatia wote mkononi mwake.


Naye mfalme wa Misri akamwondoa katika Yerusalemu, akaitoza nchi talanta mia moja za fedha, na talanta moja ya dhahabu.


Mtima wangu, mtima wangu! Naumwa katika moyo wangu wa ndani; moyo wangu umefadhaika ndani yangu; siwezi kunyamaza; kwa sababu umesikia, Ee nafsi yangu, sauti ya tarumbeta, mshindo wa vita.


Uangamivu baada ya uangamivu umetangazwa; kwa maana nchi yote imeharibika; hema zangu zimetekwa nyara ghafla, na mapazia yangu katika dakika moja.


Kwa maana watu wangu ni wapumbavu, hawanijui; ni watoto waliopungukiwa na akili, wala hawana ufahamu; ni wenye akili katika kutenda mabaya, bali katika kutenda mema hawana maarifa.


mkisema, La! Lakini tutakwenda nchi ya Misri, ambayo hatutaona vita, wala kuisikia sauti ya tarumbeta, wala kuona njaa kwa kukosa chakula; nasi tutakaa huko;


Kimbieni mpate kuwa salama, enyi wana wa Benyamini; tokeni katika Yerusalemu, pigeni tarumbeta katika Tekoa, simamisheni ishara juu ya Beth-hakeremu; kwa maana mabaya yanachungulia toka kaskazini, na uharibifu mkuu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo