Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 38:3 - Swahili Revised Union Version

3 BWANA asema hivi, Bila shaka mji huu utatiwa katika mikono ya jeshi la mfalme wa Babeli, naye atautwaa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 Mwenyezi-Mungu asema kuwa hakika mji huu utatiwa mikononi mwa jeshi la mfalme wa Babuloni na kutekwa.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

3 Mwenyezi-Mungu asema kuwa hakika mji huu utatiwa mikononi mwa jeshi la mfalme wa Babuloni na kutekwa.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 Mwenyezi-Mungu asema kuwa hakika mji huu utatiwa mikononi mwa jeshi la mfalme wa Babuloni na kutekwa.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 Tena hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: ‘Mji huu kwa hakika utatiwa mikononi mwa jeshi la mfalme wa Babeli, ambaye atauteka.’ ”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

3 Tena hili ndilo asemalo bwana: ‘Mji huu kwa hakika utatiwa mikononi mwa jeshi la mfalme wa Babeli, ambaye atauteka.’ ”

Tazama sura Nakili




Yeremia 38:3
7 Marejeleo ya Msalaba  

Maana nimeweka uso wangu juu ya mji huu niuletee mabaya, wala nisiuletee mema, asema BWANA; utatiwa katika mkono wa mfalme wa Babeli, naye atauteketeza.


BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi, Angalieni, nitazigeuza nyuma silaha za vita zilizo mikononi mwenu, ambazo kwa hizo ninyi mnapigana na mfalme wa Babeli, na Wakaldayo, wanaowahusuru nje ya kuta zenu, nami nitazikusanya pamoja katikati ya mji huu.


Yeye atakayekaa katika mji huu atakufa kwa upanga, na kwa njaa, na kwa tauni; bali yeye atakayetoka, na kujitia pamoja na Wakaldayo wanaowahusuru, yeye ataishi, na maisha yake yatakuwa nyara kwake.


Maana BWANA asema hivi, kuhusu mfalme aketiye katika kiti cha enzi cha Daudi, na kuhusu watu wote wakaao ndani ya mji huu, ndugu zenu wasiokwenda pamoja nanyi kufungwa;


Na Wakaldayo watakuja tena, na kupigana na mji huu; nao watautwaa, na kuuteketeza.


bali ukikataa kutoka kwenda kwa wakuu wa mfalme wa Babeli, basi, mji huu utatiwa katika mikono ya Wakaldayo nao watauteketeza, hata na wewe hutajiepusha na mikono yao.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo