Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 34:2 - Swahili Revised Union Version

2 BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi, Nenda ukaseme na Sedekia, mfalme wa Yuda, ukamwambie, BWANA asema hivi, Tazama, nitatia mji huu katika mikono ya mfalme wa Babeli, naye atauteketeza kwa moto;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 “Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli asema hivi: Nenda ukaongee na Sedekia, mfalme wa Yuda. Mwambie kwamba mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Nimeutia mji huu mikononi mwa mfalme wa Babuloni, naye atauteketeza kwa moto.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

2 “Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli asema hivi: Nenda ukaongee na Sedekia, mfalme wa Yuda. Mwambie kwamba mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Nimeutia mji huu mikononi mwa mfalme wa Babuloni, naye atauteketeza kwa moto.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 “Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli asema hivi: Nenda ukaongee na Sedekia, mfalme wa Yuda. Mwambie kwamba mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Nimeutia mji huu mikononi mwa mfalme wa Babuloni, naye atauteketeza kwa moto.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 “Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli: Nenda kwa Sedekia mfalme wa Yuda umwambie, ‘Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: Ninakaribia kuutia mji huu mikononi mwa mfalme wa Babeli, naye atauteketeza kwa moto.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 “Hili ndilo asemalo bwana, Mungu wa Israeli, kusema: Nenda kwa Sedekia mfalme wa Yuda umwambie, ‘Hili ndilo asemalo bwana: Ninakaribia kuutia mji huu mikononi mwa mfalme wa Babeli, naye atauteketeza kwa moto.

Tazama sura Nakili




Yeremia 34:2
14 Marejeleo ya Msalaba  

Ikawa katika mwaka wa tisa wa kutawala kwake, katika mwezi wa kumi, na siku ya kumi ya mwezi huo, Nebukadneza, mfalme wa Babeli, akaja, yeye na jeshi lake lote, kupigana na Yerusalemu, akapanga hema zake kuukabili; nao wakajenga ngome juu yake pande zote.


Akaiteketeza nyumba ya BWANA, na nyumba ya mfalme; na nyumba zote za Yerusalemu, naam, kila nyumba kubwa aliiteketeza kwa moto.


Maana nimeweka uso wangu juu ya mji huu niuletee mabaya, wala nisiuletee mema, asema BWANA; utatiwa katika mkono wa mfalme wa Babeli, naye atauteketeza.


BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi, Angalieni, nitazigeuza nyuma silaha za vita zilizo mikononi mwenu, ambazo kwa hizo ninyi mnapigana na mfalme wa Babeli, na Wakaldayo, wanaowahusuru nje ya kuta zenu, nami nitazikusanya pamoja katikati ya mji huu.


Vitachukuliwa mpaka Babeli, navyo vitakaa huko, hata siku ile nitakapovijia, asema BWANA; hapo ndipo nitakapovileta tena, na kuvirudisha mahali hapa.


Kwa maana Sedekia, mfalme wa Yuda, alikuwa amemfunga, akisema, Kwa nini unatabiri, na kusema, BWANA asema hivi, Angalia, nitatia mji huu katika mikono ya mfalme wa Babeli, naye atautwaa;


Tazama, nitawapa amri yangu, asema BWANA, na kuwarejesha kwenye mji huu; nao watapigana nao, na kuutwaa, na kuuteketeza kwa moto; nami nitaifanya miji ya Yuda kuwa ukiwa, isikaliwe na mtu.


Na watawatoa wake zako, na watoto wako wote, na kuwachukua kwa Wakaldayo; wala wewe hutapona na mikono yao, bali utakamatwa kwa mkono wa mfalme wa Babeli, nawe utakuwa sababu ya kuteketezwa mji huu.


Nao Wakaldayo wakaiteketeza nyumba ya mfalme, na nyumba za watu kwa moto, wakazibomoa kuta za Yerusalemu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo