Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 23:9 - Swahili Revised Union Version

9 Kuhusu habari za manabii. Moyo wangu ndani yangu umevunjika, Mifupa yangu yote inatikisika. Nimekuwa kama mtu aliye mlevi, Na kama mtu aliyeshindwa na divai; kwa ajili ya BWANA, na kwa ajili ya maneno yake matakatifu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 Kuhusu hao manabii wasiofaa, mimi imevunjika moyo, mifupa yangu yote inatetemeka; nimekuwa kama mlevi, kama mtu aliyelemewa na pombe, kwa sababu yake Mwenyezi-Mungu na maneno yake matakatifu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

9 Kuhusu hao manabii wasiofaa, mimi imevunjika moyo, mifupa yangu yote inatetemeka; nimekuwa kama mlevi, kama mtu aliyelemewa na pombe, kwa sababu yake Mwenyezi-Mungu na maneno yake matakatifu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 Kuhusu hao manabii wasiofaa, mimi imevunjika moyo, mifupa yangu yote inatetemeka; nimekuwa kama mlevi, kama mtu aliyelemewa na pombe, kwa sababu yake Mwenyezi-Mungu na maneno yake matakatifu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 Kuhusu manabii: Moyo wangu umevunjika ndani yangu; mifupa yangu yote inatetemeka. Nimekuwa kama mtu aliyelewa, kama mtu aliyelemewa na divai, kwa sababu ya Mwenyezi Mungu na maneno yake matakatifu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

9 Kuhusu manabii: Moyo wangu umevunjika ndani yangu; mifupa yangu yote inatetemeka. Nimekuwa kama mtu aliyelewa, kama mtu aliyelemewa na divai, kwa sababu ya bwana na maneno yake matakatifu.

Tazama sura Nakili




Yeremia 23:9
21 Marejeleo ya Msalaba  

Umewaonesha watu wako mazito, Na kutunywesha mvinyo ya kutuyumbisha.


Laumu imenivunja moyo, Nami ninaugua sana. Nikangoja aje wa kunihurumia, wala hakuna; Na wa kunifariji, wala sikumwona mtu.


Ole wa taji la kiburi la walevi wa Efraimu, na ua la uzuri wa fahari yake linalonyauka, lililo kichwani mwa bonde linalositawi, la hao walioshindwa na divai!


Ngojeni mstaajabu; fanyeni anasa zenu na kuwa vipofu; wamelewa wala si kwa mvinyo; wamewayawaya wala si kwa sababu ya kileo.


Basi, kwa sababu ya hayo, ulisikilize neno hili, ewe uliyeteswa, na kulewa, lakini si kwa mvinyo;


Ndipo niliposema, Ole wangu! Kwa maana nimepotea; kwa sababu mimi ni mtu mwenye midomo michafu, nami ninakaa kati ya watu wenye midomo michafu; na macho yangu yamemwona Mfalme, BWANA wa majeshi.


Nami nikisema, Sitamtaja, wala sitasema tena kwa jina lake; basi, ndipo moyoni mwangu kumekuwamo kama moto uwakao, uliofungwa ndani ya mifupa yangu, nami nimechoka kwa kustahimili, wala siwezi kujizuia.


Ikawa, walipoyasikia maneno hayo yote, wakatazamana kwa hofu, wakamwambia Baruku, Hatuna budi kumwambia mfalme maneno haya yote.


Manabii wanatabiri uongo, na makuhani wanatawala kwa msaada wa hao; na watu wangu wanapenda mambo yawe hivyo. Nanyi mtafanya nini mwisho wake?


Laiti ningeweza kujifariji, nisione huzuni! Moyo wangu umezimia ndani yangu.


Laiti kichwa changu kingekuwa maji, na macho yangu kuwa chemchemi ya machozi, ili nipate kulia mchana na usiku kwa ajili yao waliouawa wa binti ya watu wangu!


Amenijaza uchungu, Amenikinaisha kwa pakanga.


Bwana MUNGU asema hivi; Ole wao manabii wajinga, wanaoifuata roho yao wenyewe, wala hawakuona neno lolote!


BWANA akamwambia, Pita kati ya mji, kati ya Yerusalemu, ukatie alama katika vipaji vya nyuso vya watu wanaopiga kite na kulia kwa sababu ya machukizo yote yanayofanyika kati yake.


Waueni kabisa, wazee, na viijana, na wasichana, na watoto wachanga, na wanawake; lakini msimkaribie mtu yeyote mwenye hiyo alama; tena anzeni katika patakatifu pangu. Basi, wakaanza kwa wazee waliokuwa mbele ya nyumba.


Na mimi, Danieli, nikazimia, nikaugua siku kadhaa; kisha nikaondoka, nikatenda shughuli za mfalme; nami niliyastajabia yale maono, ila hakuna aliyeyafahamu.


Nikasikia, na tumbo langu likatetemeka, Midomo yangu ikatikisika kwa sauti ile; Ubovu ukaingia mifupani mwangu, Nikatetemeka katika mahali pangu; Ili nipate kuingoja ile siku ya dhiki, Kundi lao washambuliao wakweapo juu ya watu.


Nami nilikuwa hai hapo kwanza bila sheria; ila ilipokuja ile amri, dhambi ilihuika, nami nikafa.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo