Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 23:7 - Swahili Revised Union Version

7 Kwa hiyo, angalia, siku zinakuja, asema BWANA, ambapo hawatasema tena, Aishivyo BWANA, aliyewatoa wana wa Israeli katika nchi ya Misri;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

7 “Kwa hiyo siku zaja, nasema mimi Mwenyezi-Mungu, ambapo watu hawataapa tena kwa kusema, ‘Kama aishivyo Mwenyezi-Mungu aliyewatoa watu wa Israeli nchini Misri’,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

7 “Kwa hiyo siku zaja, nasema mimi Mwenyezi-Mungu, ambapo watu hawataapa tena kwa kusema, ‘Kama aishivyo Mwenyezi-Mungu aliyewatoa watu wa Israeli nchini Misri’,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

7 “Kwa hiyo siku zaja, nasema mimi Mwenyezi-Mungu, ambapo watu hawataapa tena kwa kusema, ‘Kama aishivyo Mwenyezi-Mungu aliyewatoa watu wa Israeli nchini Misri’,

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

7 Mwenyezi Mungu asema, “Hivyo basi, siku zinakuja, ambapo watu hawatasema tena, ‘Hakika kama Mwenyezi Mungu aishivyo, aliyewapandisha Waisraeli kutoka Misri,’

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

7 “Hivyo basi, siku zinakuja, wakati ambapo watu hawatasema tena, ‘Hakika kama bwana aishivyo, aliyewapandisha Waisraeli kutoka Misri,’

Tazama sura Nakili




Yeremia 23:7
9 Marejeleo ya Msalaba  

Na itakuwa katika siku hiyo, Bwana atapeleka mkono wake mara ya pili, ili ajipatie watu wake watakaosalia, kutoka Ashuru, na kutoka Misri, na kutoka Pathrosi, na kutoka Kushi, na kutoka Elamu, na kutoka Shinari, na kutoka Hamathi, na kutoka visiwa vya bahari.


Usiogope; maana mimi ni pamoja nawe; nitaleta wazao wako toka mashariki, nitakukusanya toka magharibi;


Nami nitakusanya mabaki ya kundi langu, katika nchi zile zote nilizowafukuza, nami nitawaleta tena mazizini mwao; nao watazaa na kuongezeka.


Kwa maana, tazama, siku zinakuja, asema BWANA, nitakapowarejesha watu wangu wa Israeli na Yuda waliofungwa, asema BWANA; nami nitawarudisha hadi katika nchi niliyowapa baba zao, nao wataimiliki.


Kwa kuwa mmetwaa fedha yangu na dhahabu yangu, nanyi mmevichukua vitu vyangu vyema vipendezavyo, na kuviingiza katika hekalu zenu;


Kama katika siku zile za kutoka kwako katika nchi ya Misri nitamwonesha mambo ya ajabu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo