Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 2:2 - Swahili Revised Union Version

2 Nenda ukalie masikioni mwa Yerusalemu, ukisema, BWANA asema hivi, Nakukumbuka, hisani ya ujana wako, upendo wa wakati wa kuposwa kwako; Jinsi ulivyonifuata huko jangwani, katika nchi isiyopandwa mbegu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 “Nenda ukawatangazie waziwazi wakazi wote wa Yerusalemu kuwa mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Naukumbuka uaminifu wako ulipokuwa kijana, jinsi ulivyonipenda kama mchumba wako, ulivyonifuata jangwani kwenye nchi ambayo haikupandwa kitu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

2 “Nenda ukawatangazie waziwazi wakazi wote wa Yerusalemu kuwa mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Naukumbuka uaminifu wako ulipokuwa kijana, jinsi ulivyonipenda kama mchumba wako, ulivyonifuata jangwani kwenye nchi ambayo haikupandwa kitu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 “Nenda ukawatangazie waziwazi wakazi wote wa Yerusalemu kuwa mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Naukumbuka uaminifu wako ulipokuwa kijana, jinsi ulivyonipenda kama mchumba wako, ulivyonifuata jangwani kwenye nchi ambayo haikupandwa kitu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 “Nenda ukahubiri masikioni mwa watu wa Yerusalemu: “Hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi Mungu: “ ‘Nakumbuka moyo wako wa uchaji katika ujana wako, jinsi ulivyonipenda kama bibi arusi na kunifuata katika jangwa lile lote, katika nchi isiyopandwa mbegu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 “Nenda ukahubiri masikioni mwa watu wa Yerusalemu: “ ‘Nakumbuka moyo wako wa uchaji katika ujana wako, jinsi ulivyonipenda kama bibi arusi na kunifuata katika jangwa lile lote, katika nchi isiyopandwa mbegu.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

2 Nenda ukalie masikioni mwa Yerusalemu, ukisema, BWANA asema hivi, Nakukumbuka, hisani ya ujana wako, upendo wa wakati wa kuposwa kwako; Jinsi ulivyonifuata huko jangwani, katika nchi isiyopandwa mbegu.

Tazama sura Nakili




Yeremia 2:2
39 Marejeleo ya Msalaba  

Mara nyingi wamenitesa tangu ujana wangu, Israeli na aseme sasa,


Israeli akaiona ile kazi kubwa aliyoifanya BWANA juu ya Wamisri, ndipo hao watu wakamcha BWANA, wakamwamini BWANA, na Musa mtumishi wake.


Musa akasema, Ndilo litakalokuwa, hapo BWANA atakapowapa nyama wakati wa jioni mle, na asubuhi mikate hata mkakinai; kwa kuwa BWANA asikia manung'uniko yenu mliyomnung'unikia yeye; na sisi tu nani? Manung'uniko yenu hayakuwa juu yetu sisi, ila juu ya BWANA.


Hekima hulia kwa sauti katika njia kuu, Hupaza sauti yake katika viwanja;


Tokeni, enyi binti za Sayuni, Mtazameni Mfalme Sulemani, Amevaa taji alilovikwa na mamaye, Siku ya posa yake, Siku ya furaha ya moyo wake.


Ni nani huyu apandaye kutoka nyikani, Mfano wake ni nguzo za moshi; Afukizwa manemane na ubani, Na mavumbi ya manukato yote ya mchuuzi?


Piga kelele, usiache, Paza sauti yako kama tarumbeta; Uwahubirie watu wangu kosa lao, Na nyumba ya Yakobo dhambi zao.


Naye BWANA akaniambia, Hubiri maneno haya yote katika miji ya Yuda, na katika njia kuu za Yerusalemu, ukisema, Yasikieni maneno ya maagano haya, mkayafanye.


ukatoke uende mpaka bonde la mwana wa Hinomu lililo karibu na mahali pa kuingia kwa lango la vigae, ukahubiri huko maneno nitakayokuambia,


Neno la BWANA likanijia, kusema,


Wala hawakusema, Yuko wapi BWANA, aliyetutoa katika nchi ya Misri; akatuongoza jangwani, katika nchi ya ukame na mashimo, katika nchi ya kiu na ya kivuli cha mauti, katika nchi ambayo ndani yake hapiti mtu, wala haikukaliwa na watu?


Je, tokea wakati huu hutanililia, Ee Baba yangu, wewe u kiongozi wa ujana wangu?


Simama langoni pa nyumba ya BWANA, ukatangaze hapo neno hili, ukisema, Sikilizeni neno la BWANA, ninyi nyote wa Yuda, mnaoingia katika malango haya ili kumwabudu BWANA.


Na katika machukizo yako yote, na mambo yako ya kikahaba, hukuzikumbuka siku za ujana wako, ulipokuwa uchi, bila mavazi, ukawa ukigaagaa katika damu yako.


Walakini nitalikumbuka agano langu nililolifanya pamoja nawe, katika siku za ujana wako, nami nitaweka imara agano la milele pamoja nawe.


Basi, nilipopita karibu nawe, nikakutazama; tazama, wakati wako ulikuwa wakati wa upendo; nikatandika upindo wa vazi langu juu yako, nikakufunika uchi wako; naam, nilikuapia, nikafanya agano nawe, asema Bwana MUNGU, ukawa wangu.


Lakini aliongeza uzinzi wake, akikumbuka siku za ujana wake, alipofanya mambo ya kikahaba katika nchi ya Misri.


nao walizini huko Misri; walizini wakati wa ujana wao; huko vifua vyao vilishikwashikwa, na matiti yao yakatomaswa wakapoteza ubikira wao.


Wala hakuyaacha mambo yake ya kikahaba tangu siku za Misri, kwa maana wakati wa ujana wake walilala naye, wakayabana matiti ya ubikira wake wakamwaga uzinzi wao juu yake.


Israeli alipokuwa mtoto, nilikuwa nikimpenda, nikamwita mwanangu atoke Misri.


Nami nitampa mashamba yake ya mizabibu toka huko, na bonde la Akori kuwa mlango wa tumaini; naye ataniitikia huko, kama siku zile za ujana wake, na kama siku ile alipopanda kutoka nchi ya Misri.


Kwa maana nitayaondoa majina ya Mabaali kinywani mwake, wala hawatatajwa tena kwa majina yao.


Naye atawafuata wapenzi wake, lakini hatawapata; atawatafuta, lakini hatawaona; ndipo atakaposema, Nitakwenda nikamrudie mume wangu wa kwanza; kwa maana hali yangu ya zamani ilikuwa njema kuliko hali yangu ya sasa.


Tia baragumu kinywani mwako. Kama tai, anakuja juu ya nyumba ya BWANA; kwa sababu wamelivunja agano langu, wameiasi sheria yangu.


Mimi nilimkuta Israeli kama zabibu nyikani; nami niliwaona baba zenu kama matunda ya mtini yaliyoiva kwanza, msimu wake wa kwanza; lakini walikwenda Baal-Peori, wakajiweka wakfu kwa kitu cha aibu, wakawa chukizo kama kitu kile walichokipenda.


Ondoka, uende Ninawi, mji ule mkubwa, ukapige kelele juu yake; kwa maana uovu wao umepanda juu mbele zangu.


Mwenye masikio, na asikie.


Mtu mmoja katika mkutano akamwambia, Mwalimu, mwambie ndugu yangu anigawie urithi wetu.


Kwa kuwa BWANA, Mungu wako, amekubariki katika kazi yote ya mkono wako; amejua ulivyotembea katika jangwa kubwa hili; miaka arubaini hii alikuwa nawe BWANA, Mungu wako; hukukosa kitu.


Hakika awapenda hayo makabila ya watu; Watakatifu wake wote wamo mkononi mwako; Nao waliketi miguuni pako; Watapokea kila mmoja katika maneno yako.


Nawe utaikumbuka njia ile yote BWANA, Mungu wako aliyokuongoza miaka hii arubaini katika jangwa, ili akunyenyekeze, kukujaribu kuyajua yaliyo moyoni mwako, kwamba utashika amri zake, au sivyo.


Enyi wazinzi, hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu? Basi kila atakaye kuwa rafiki wa dunia hujifanya kuwa adui wa Mungu.


Lakini nina neno juu yako, ya kwamba umeuacha upendo wako wa kwanza.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo