Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 19:7 - Swahili Revised Union Version

7 Nami nitalitangua shauri la Yuda na Yerusalemu mahali hapa; nami nitawaangusha kwa upanga mbele za adui zao, na kwa mkono wa watu watafutao roho zao; na mizoga yao nitawapa ndege wa angani na wanyama wakali wa nchi, iwe chakula chao.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

7 Na papa hapa nitaivuruga mipango ya Yuda na Yerusalemu. Nitawafanya watu wao washindwe na kuuawa na maadui zao vitani na kuangamizwa na wale wanaowawinda. Maiti zao nitawaachia ndege wa anga na wanyama wa porini kuwa chakula chao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

7 Na papa hapa nitaivuruga mipango ya Yuda na Yerusalemu. Nitawafanya watu wao washindwe na kuuawa na maadui zao vitani na kuangamizwa na wale wanaowawinda. Maiti zao nitawaachia ndege wa anga na wanyama wa porini kuwa chakula chao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

7 Na papa hapa nitaivuruga mipango ya Yuda na Yerusalemu. Nitawafanya watu wao washindwe na kuuawa na maadui zao vitani na kuangamizwa na wale wanaowawinda. Maiti zao nitawaachia ndege wa anga na wanyama wa porini kuwa chakula chao.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

7 “ ‘Nitaiharibu mipango ya Yuda na Yerusalemu mahali hapa. Nitawafanya waanguke kwa upanga mbele ya adui zao, katika mikono ya wale wanaotafuta uhai wao, nami nitaitoa mizoga yao kuwa chakula cha ndege wa angani na wanyama wa nchi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

7 “ ‘Nitaiharibu mipango ya Yuda na Yerusalemu mahali hapa. Nitawafanya waanguke kwa upanga mbele ya adui zao, katika mikono ya wale watafutao uhai wao, nami nitaitoa mizoga yao kuwa chakula cha ndege wa angani na wanyama wa nchi.

Tazama sura Nakili




Yeremia 19:7
32 Marejeleo ya Msalaba  

Nami nitawatupa mabaki ya urithi wangu, na kuwatia mikononi mwa adui zao; nao watakuwa nyara na mateka kwa adui zao wote;


Hapana hekima, wala ufahamu, Wala shauri, juu ya BWANA.


kwa sababu hiyo mimi nitafanya tena kazi ya ajabu kati ya watu hawa, kazi ya ajabu na mwujiza; na akili za watu wao wenye akili zitapotea, na ufahamu wa wenye busara wao utafichwa.


Fanyeni shauri pamoja, nalo litabatilika; Semeni neno, lakini halitasimama; Kwa maana Mungu yu pamoja nasi.


Kisha itakuwa, hapo watakapokuambia, Tutoke, tuende wapi? Utawaambia, BWANA asema hivi, Walioandikiwa kufa, watakwenda kufa; au kufa kwa upanga, watakufa kwa upanga; au kufa kwa njaa, watakufa kwa njaa, au kutekwa nyara, watakuwa mateka.


Mwanamke aliyezaa watoto saba anazimia; ametoa roho; jua lake limekuchwa, ikiwa bado ni wakati wa mchana; ameaibika na kutwezwa; na mabaki yao nitawatoa kwa upanga mbele ya adui zao, asema BWANA.


watakufa kwa maradhi mabaya; hawataliliwa, wala hawatazikwa; watakuwa kama samadi juu ya uso wa nchi; nao wataangamizwa kwa upanga, na kwa njaa; na mizoga yao itakuwa chakula cha ndege wa angani, na cha wanyama wa nchi.


Kwa sababu hiyo, uwatoe watoto wao waone njaa, uwatoe nguvu za upanga ziwapate; wake zao wafiwe na watoto wao, na kufiwa na waume zao; wanaume wao wauawe, na vijana wao wapigwe kwa upanga vitani.


Na baada ya hayo, asema BWANA, nitamtia Sedekia, mfalme wa Yuda, na watumishi wake, na watu wote waliosalia ndani ya mji huu, baada ya tauni ile, na upanga, na njaa, katika mkono wa Nebukadneza, mfalme wa Babeli, na katika mikono ya adui zao, na katika mikono ya watu wale wanaowatafuta roho zao; naye atawaua kwa ukali wa upanga; hatawaachilia, wala hatawahurumia, wala hatawarehemu.


Atazikwa maziko ya punda, akibururwa, na kutupwa nje ya malango ya Yerusalemu.


nami nitakutia katika mikono ya watu wale wakutafutao roho yako, na katika mikono yao unaowaogopa, naam, katika mikono ya Nebukadneza, mfalme wa Babeli, na katika mikono ya Wakaldayo.


Basi, BWANA asema hivi, Tazama, nitautia mji huu katika mikono ya Wakaldayo, na katika mikono ya Nebukadneza, mfalme wa Babeli, naye atautwaa;


mimi nitawatia katika mikono ya adui zao, na katika mikono ya watu wale wanaowatafuta roho zao, na mizoga yao itakuwa ni chakula cha ndege wa mbinguni, na cha wanyama wakali wa nchi.


nami nitawatia katika mikono ya hao wanaowatafuta roho zao, na katika mikono ya Nebukadneza, mfalme wa Babeli, na katika mikono ya watumishi wake; na baada ya hayo itakaliwa na watu, kama katika siku za kale, asema BWANA.


Na mizoga ya watu hawa itakuwa chakula cha ndege wa angani, na cha wanyama wa nchi; wala hapana mtu atakayewafukuza.


nao wataitawanya mbele ya jua, na mwezi, na jeshi lote la mbinguni, walivyovipenda, na kuvitumikia, na kuandamana navyo, na kuvitafuta, na kuviabudu haitakusanywa pamoja tena, wala kuzikwa; itakuwa ni samadi juu ya uso wa nchi.


Mwasemaje, Sisi tuna akili, na Torati ya BWANA tunayo pamoja nasi? Lakini, tazama, kalamu yenye uongo ya waandishi imeifanya kuwa uongo.


Wenye hekima wametahayari, wamefadhaika na kushikwa; tazama, wamelikataa neno la BWANA, wana akili gani ndani yao?


Ni nani asemaye neno nalo likafanyika, Ikiwa Bwana hakuliagiza?


Nami nitauelekeza uso wangu kinyume chenu, nanyi mtapigwa mbele ya adui zenu; hao wawachukiao watatawala juu yenu; nanyi mtakimbia wakati ambao hapana awafukuzaye.


Nami nitaleta upanga juu yenu, utakaopatiliza kisasi cha hilo agano; nanyi mtakutanishwa ndani ya miji yenu; nami nitaleta tauni kati yenu; nanyi mtatiwa mikononi mwa adui.


Basi, je! Twaibatilisha sheria kwa imani hiyo? La hasha! Kinyume cha hayo twaithibitisha sheria.


Maana ikiwa wale wa sheria ndio warithi, imani imekuwa bure, na ahadi imebatilika.


Siku hii ya leo BWANA atakuua mkononi mwangu, nami nitakupiga, na kukuondolea kichwa chako, nami leo nitawapa ndege wa angani na wanyama wa nchi mizoga ya majeshi ya Wafilisti, ili kwamba dunia nzima wajue ya kuwa yuko Mungu katika Israeli.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo