Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 17:5 - Swahili Revised Union Version

5 BWANA asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake Na moyoni mwake amemwacha BWANA.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Alaaniwe mtu anayemtegemea binadamu, mtu ambaye anategemea nguvu za binadamu, mtu ambaye moyo wake umeniacha mimi Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

5 Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Alaaniwe mtu anayemtegemea binadamu, mtu ambaye anategemea nguvu za binadamu, mtu ambaye moyo wake umeniacha mimi Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Alaaniwe mtu anayemtegemea binadamu, mtu ambaye anategemea nguvu za binadamu, mtu ambaye moyo wake umeniacha mimi Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: “Amelaaniwa yeye amtegemeaye mwanadamu, amtegemeaye mwenye mwili kwa ajili ya nguvu zake, ambaye moyo wake umemwacha Mwenyezi Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 Hili ndilo asemalo bwana: “Amelaaniwa yeye amtegemeaye mwanadamu, ategemeaye mwenye mwili kwa ajili ya nguvu zake, ambaye moyo wake umemwacha bwana.

Tazama sura Nakili




Yeremia 17:5
16 Marejeleo ya Msalaba  

Katika mwaka wa thelathini na tisa wa kumiliki kwake, Asa akashikwa na ugonjwa wa miguu; ugonjwa wake ukazidi sana; lakini hakumtafuta BWANA katika ugonjwa wake, bali alitafuta msaada wa waganga.


kwake upo mkono wa mwili; ila kwetu yupo BWANA, Mungu wetu, kutusaidia, na kutupigania mapigano yetu. Na watu wakayategemea maneno ya Hezekia, mfalme wa Yuda.


Maana nimezishika njia za BWANA, Wala sikumwasi Mungu wangu.


Hakika binadamu ni ubatili, Na wenye cheo ni uongo, Katika mizani huinuka; Wote pamoja ni hafifu kuliko ubatili.


Mwacheni mwanadamu ambaye pumzi yake iko katika mianzi ya pua yake; kwa maana wanafaa kitu gani?


Nao watafadhaika, na kuona haya kwa ajili ya Kushi, matumaini yao, na Misri, utukufu wao.


Tazama, unaitumainia fimbo ya mwanzi huu uliovunjika, yaani, Misri, ambayo, mtu akitegemea juu yake, humwingia mkononi na kumchoma; ndivyo alivyo Farao, mfalme wa Misri, kwa wote wamtumainio.


Naam, kweli imepunguka kabisa, na yeye auachaye uovu ajifanya kuwa mateka; naye BWANA akaona hayo, akachukizwa kwa kuwa hapana hukumu ya haki.


ukawaambie, BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi, Na alaaniwe mtu asiyeyasikia maneno ya maagano haya,


Na hao wa kwenu watakaookoka watanikumbuka kati ya mataifa, watakakochukuliwa mateka, jinsi nilivyoiponda mioyo yao ya kikahaba, iliyoniacha, na macho yao, yaendayo kufanya uasherati na vinyago vyao; nao watajichukia nafsi zao machoni pao wenyewe, kwa sababu ya mabaya yao yote, waliyoyatenda kwa machukizo yao yote.


Hapo kwanza BWANA aliponena kwa kinywa cha Hosea, BWANA alimwambia Hosea, Nenda ukatwae mke wa uzinzi, na watoto wa uzinzi; kwa maana nchi hii inafanya uzinzi mwingi, kwa kumwacha BWANA.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo