Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 10:1 - Swahili Revised Union Version

1 Enyi nyumba ya Israeli, lisikieni neno awaambialo BWANA;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Sikilizeni neno analowaambieni Mwenyezi-Mungu, enyi Waisraeli!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Sikilizeni neno analowaambieni Mwenyezi-Mungu, enyi Waisraeli!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Sikilizeni neno analowaambieni Mwenyezi-Mungu, enyi Waisraeli!

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Sikieni lile Mwenyezi Mungu anasema nanyi, ee nyumba ya Israeli.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Sikieni lile ambalo bwana, anena nanyi ee nyumba ya Israeli.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

1 Enyi nyumba ya Israeli, lisikieni neno awaambialo BWANA;

Tazama sura Nakili




Yeremia 10:1
16 Marejeleo ya Msalaba  

Mikaya akasema, Sikia basi neno la BWANA; Nilimwona BWANA ameketi katika kiti chake cha enzi, na jeshi lote la mbinguni wamesimama upande wa mkono wake wa kulia na wa kushoto.


Sikieni, enyi watu wangu, nami nitanena, Mimi nitakushuhudia, Israeli; Mimi ndimi niliye MUNGU, Mungu wako.


Lisikieni neno la BWANA, enyi waamuzi wa Sodoma; tegeni masikio msikie sheria ya Mungu wetu, enyi watu wa Gomora.


Basi, lisikieni neno la BWANA, enyi watu wenye dharau, mnaowatawala watu hawa walio ndani ya Yerusalemu.


Basi, mtamlinganisha Mungu na nani? Au mtamfananisha na mfano wa namna gani?


BWANA, Mfalme wa Israeli, Mkombozi wako, BWANA wa majeshi, asema hivi; Mimi ni wa kwanza, na mimi ni wa mwisho; zaidi yangu mimi hapana Mungu.


BWANA asema hivi, Msijifunze njia ya mataifa, wala msishangae kwa sababu ya ishara za mbinguni; maana mataifa hushangaa kwa sababu ya ishara hizo.


Lisikieni neno la BWANA, ninyi nyumba ya Yakobo, na ninyi, jamaa zote za nyumba ya Israeli.


ya kwamba, Sikia neno la BWANA, Ee mfalme wa Yuda; wewe uketiye katika kiti cha enzi cha Daudi, wewe, na watumishi wako, na watu wako wote waingiao kwa malango haya;


basi, lisikieni neno la BWANA, enyi mabaki ya Yuda; BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Ikiwa mnakaza nyuso zenu kuingia Misri, na kwenda kukaa huko;


Misri, na Yuda, na Edomu, na wana wa Amoni, na Moabu, na wote wenye kunyoa denge, wakaao nyikani; maana mataifa hayo yote hawana tohara, wala nyumba yote ya Israeli hawakutahiriwa mioyo yao.


Lisikieni neno la BWANA, enyi wana wa Israeli; kwa maana BWANA ana shutuma nao wakaao katika nchi, kwa sababu hapana kweli, wala fadhili, wala kumjua Mungu katika nchi.


Basi, sasa lisikie neno la BWANA; Wewe unasema, Usitabiri juu ya Israeli, wala usitoe neno lako juu ya nyumba ya Isaka;


Kwa sababu hiyo sisi nasi tunamshukuru Mungu bila kukoma, kwa kuwa, mlipopata lile neno la ujumbe wa Mungu mlilolisikia kwetu, mlilipokea si kama neno la wanadamu, bali kama neno la Mungu; na kwa kweli ndivyo lilivyo; litendalo kazi pia ndani yenu ninyi mnaoamini.


Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho anayaambia makanisa.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo