Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Walawi 9:3 - Swahili Revised Union Version

3 Nawe utawaambia wana wa Israeli, ukisema, Twaeni mbuzi dume awe sadaka ya dhambi; na mwana-ng'ombe, na mwana-kondoo, wote wa mwaka wa kwanza, wakamilifu, kwa sadaka ya kuteketezwa;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 Waambie Waisraeli wachukue beberu mmoja kwa ajili ya sadaka ya kuondoa dhambi, na ndama mmoja na mwanakondoo mmoja wote wa umri wa mwaka mmoja na wasio na dosari kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

3 Waambie Waisraeli wachukue beberu mmoja kwa ajili ya sadaka ya kuondoa dhambi, na ndama mmoja na mwanakondoo mmoja wote wa umri wa mwaka mmoja na wasio na dosari kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 Waambie Waisraeli wachukue beberu mmoja kwa ajili ya sadaka ya kuondoa dhambi, na ndama mmoja na mwanakondoo mmoja wote wa umri wa mwaka mmoja na wasio na dosari kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa,

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 Kisha waambie Waisraeli: ‘Chukueni beberu kwa ajili ya sadaka ya dhambi, na ndama na mwana-kondoo, wote wawili wawe wa umri wa mwaka mmoja, na wasio na dosari, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

3 Kisha waambie Waisraeli: ‘Chukueni mbuzi dume kwa ajili ya sadaka ya dhambi, na ndama na mwana-kondoo, wote wawili wawe wa umri wa mwaka mmoja, na wasio na dosari, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa,

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

3 Nawe utawaambia wana wa Israeli, ukisema, Twaeni mbuzi dume awe sadaka ya dhambi; na mwana-ng'ombe, na mwana-kondoo, wote wa mwaka mmoja, wakamilifu, kwa sadaka ya kuteketezwa;

Tazama sura Nakili




Walawi 9:3
22 Marejeleo ya Msalaba  

Wakaitwaa kanzu ya Yusufu, wakachinja mwana-mbuzi, na kuichovya kanzu katika damu.


Nao wakatoa ahadi ya kwamba wataachana na wake zao; na kwa kuwa walikuwa na hatia, wakatoa kondoo dume kwa hatia yao.


Na katika kuiweka wakfu nyumba ya Mungu, wakatoa sadaka, ng'ombe mia moja, na kondoo dume mia mbili, na wana-kondoo mia nne; tena wakatoa mbuzi dume kumi na wawili, kuwa sadaka ya dhambi kwa ajili ya Waisraeli wote, kwa hesabu ya makabila ya Israeli.


Mwana-kondoo wenu atakuwa hana dosari, wa kiume wa mwaka mmoja; mtamtwaa katika kondoo au katika mbuzi.


Lakini BWANA aliridhika kumchubua; Amemhuzunisha; Utakapofanya nafsi yake kuwa dhabihu kwa dhambi, Ataona uzao wake, ataishi siku nyingi, Na mapenzi ya BWANA yatafanikiwa mkononi mwake;


Kisha Musa akamtafuta sana huyo mbuzi wa sadaka ya dhambi, naye, tazama, alikuwa amekwisha kuteketezwa; naye akawakasirikia hao Eleazari na Ithamari, wana wa Haruni, hao waliobaki, akawaambia,


Kisha hizo siku za kutakaswa kwake zitakapotimia, kwa ajili ya mtoto wa kiume, au kwa ajili ya mtoto wa kike ataleta mwana-kondoo wa mwaka mmoja kuwa sadaka ya kuteketezwa na kinda la njiwa, au hua, kuwa sadaka ya dhambi, awalete mlangoni pa hema ya kukutania, na kumpa kuhani;


Kisha siku ya nane atachukua wana-kondoo wawili wa kiume wasio na dosari, na mwana-kondoo mmoja wa kike wa mwaka wa kwanza asiye na dosari, na sehemu tatu za kumi za efa moja ya unga mwembamba kuwa sadaka ya unga, kuchanganywa na mafuta, na logi moja ya mafuta.


Kisha atamchinja yule mbuzi wa sadaka ya dhambi, aliye kwa ajili ya watu, na kuileta damu yake ndani ya pazia, na kwa damu hiyo atafanya kama alivyofanya kwa damu ya ng'ombe, na kuinyunyiza juu ya kiti cha rehema, na mbele ya kiti cha rehema,


Kisha atatwaa mikononi mwa mkutano wa Waisraeli mbuzi wawili wa kiume, kwa sadaka ya dhambi; na kondoo dume kwa sadaka ya kuteketezwa.


Na siku hiyo mtakayoutikisa mganda, mtamsongeza mwana-kondoo wa kiume asiye na dosari wa mwaka wa kwanza, awe sadaka ya kuteketezwa kwa BWANA.


akijulishwa hiyo dhambi yake aliyoifanya, ataleta mbuzi dume asiye na dosari awe matoleo yake;


kama kuhani aliyetiwa mafuta akifanya dhambi, hata analeta hatia juu ya watu; ndipo na atoe kwa ajili ya dhambi yake aliyoifanya, na kumsongeza kwa BWANA ng'ombe dume mchanga mkamilifu, kuwa ni sadaka ya dhambi.


akamwambia Haruni, Twaa wewe mwana-ng'ombe wa kiume awe sadaka ya dhambi, na kondoo dume wa sadaka ya kuteketezwa, wakamilifu, ukawasongeze mbele ya BWANA.


na ng'ombe dume, na kondoo dume, kwa sadaka za amani, ili kuwachinja mbele za BWANA; na sadaka ya unga uliochanganywa na mafuta; kwa maana, BWANA hivi leo atawatokea.


Maana yale yasiyowezekana kwa sheria, kwa vile ilivyokuwa dhaifu kwa sababu ya mwili, Mungu, kwa kumtuma Mwanawe mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa sababu ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili;


Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika Yeye.


ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili yetu, ili atukomboe na maasi yote, na kujisafishia watu wake mwenyewe walio na bidii katika matendo mema.


Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe hai kwa mambo ya haki; na kwa kupigwa kwake mliponywa.


Kwa maana Kristo naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio haki, ili atulete kwa Mungu; akauawa kimwili, lakini akahuishwa kiroho,


Nao waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa hicho kitabu na kuifungua mihuri yake; kwa kuwa ulichinjwa, ukawa fidia kwa Mungu na kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo