Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Walawi 7:7 - Swahili Revised Union Version

7 Kama hiyo sadaka ya dhambi ilivyo, na sadaka ya hatia ni vivyo hivyo; sheria yake ni moja; huyo kuhani afanyaye upatanisho kwayo, ndiye atakayekuwa nayo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

7 Sheria ni moja kuhusu sadaka ya kuondoa hatia na sadaka ya kuondoa dhambi: Kuhani anayefanya ibada ya upatanisho ndiye atakayeichukua.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

7 Sheria ni moja kuhusu sadaka ya kuondoa hatia na sadaka ya kuondoa dhambi: Kuhani anayefanya ibada ya upatanisho ndiye atakayeichukua.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

7 Sheria ni moja kuhusu sadaka ya kuondoa hatia na sadaka ya kuondoa dhambi: kuhani anayefanya ibada ya upatanisho ndiye atakayeichukua.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

7 “ ‘Sheria hii ya sadaka ya hatia ni sawasawa na ile ya sadaka ya dhambi: Nyama ya yule mnyama aliyetolewa sadaka ni ya yule kuhani anayesimamia ibada ya upatanisho.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

7 “ ‘Sheria hii ya sadaka ya hatia ni sawasawa na ile ya sadaka ya dhambi: Nyama ya yule mnyama aliyetolewa sadaka ni ya yule kuhani anayesimamia ibada ya upatanisho.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

7 Kama hiyo sadaka ya dhambi ilivyo, na sadaka ya hatia ni vivyo hivyo; sheria yake ni moja; huyo kuhani afanyaye upatanisho kwayo, ndiye atakayekuwa nayo.

Tazama sura Nakili




Walawi 7:7
11 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini fedha ya matoleo ya kosa, na fedha ya matoleo ya dhambi, haikuletwa nyumbani mwa BWANA; hiyo ilikuwa ya makuhani wenyewe.


Ndipo akakwea Hazaeli mfalme wa Shamu akapigana na Gathi, akautwaa; Hazaeli akaelekeza uso ili akwee kwenda Yerusalemu.


kisha atamchinja huyo mwana-kondoo mahali hapo wachinjiapo sadaka ya dhambi na sadaka ya kuteketezwa, ndani ya mahali patakatifu; kwa kuwa kama hiyo sadaka ya dhambi ilivyo ya kuhani, ndivyo ilivyo sadaka ya hatia; ni takatifu sana;


Na hicho kitakachosalia katika sadaka ya unga kitakuwa cha Haruni na wanawe; ni kitu kitakatifu sana katika sadaka zilizosongezwa kwa BWANA kwa njia ya moto.


na huo uliosalia wa ile sadaka ya unga utakuwa ni wa Haruni na wanawe; ni kitu kitakatifu sana katika sadaka zilizotolewa kwa BWANA kwa njia ya moto.


Hautaokwa kwa chachu. Nimewapa kuwa sehemu yao katika matoleo yangu yasongezwayo kwa njia ya moto; ni kitu kitakatifu sana, kama hiyo sadaka ya dhambi, na kama hiyo sadaka ya hatia.


Tena kuhani atakayesongeza sadaka ya kuteketezwa ya mtu awaye yote, huyo kuhani atatwaa awe nayo ngozi ya huyo mnyama wa sadaka ya kuteketezwa aliyemsongeza.


Lakini ikiwa mtu huyo hana jamaa ya karibu ambaye inampasa kurudishiwa kwa ajili ya hiyo hatia, kile kitakachorudishwa kwa BWANA kwa hiyo hatia kitakuwa cha kuhani, pamoja na kondoo dume wa upatanisho, ambaye kwa huyo utafanywa upatanisho kwa ajili yake.


Waangalieni hao Waisraeli walivyokuwa kwa jinsi ya mwili; wale wazilao dhabihu, je! Hawana shirika na madhabahu?


Hamjui ya kuwa wale wazifanyao kazi za hekaluni hula katika vitu vya hekalu, na wale waihudumiayo madhabahu huwa na fungu lao katika vitu vya madhabahu?


Tufuate:

Matangazo


Matangazo