Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Walawi 7:30 - Swahili Revised Union Version

30 mikono yake mwenyewe itamletea hizo sadaka za kusongezwa kwa moto; mafuta yake pamoja na kidari atavileta, ili kwamba hicho kidari kitikiswe kuwa sadaka ya kutikiswa mbele ya BWANA.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

30 Atamletea kwa mikono yake mwenyewe kama sadaka ya kuteketezwa kwa moto. Ataleta mafuta yake pamoja na kidari ambacho atafanya nacho ishara ya kumtolea Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

30 Atamletea kwa mikono yake mwenyewe kama sadaka ya kuteketezwa kwa moto. Ataleta mafuta yake pamoja na kidari ambacho atafanya nacho ishara ya kumtolea Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

30 Atamletea kwa mikono yake mwenyewe kama sadaka ya kuteketezwa kwa moto. Ataleta mafuta yake pamoja na kidari ambacho atafanya nacho ishara ya kumtolea Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

30 Ataleta sadaka kwa mikono yake mwenyewe iliyotolewa kwa Mwenyezi Mungu kwa moto; ataleta mafuta ya huyo mnyama pamoja na kidari, naye atainua hicho kidari mbele za Mwenyezi Mungu kuwa sadaka ya kuinuliwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

30 Ataleta sadaka kwa mikono yake mwenyewe iliyotolewa kwa bwana kwa moto; ataleta mafuta ya huyo mnyama pamoja na kidari, naye atainua hicho kidari mbele za bwana kuwa sadaka ya kuinuliwa.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

30 mikono yake mwenyewe itamletea hizo sadaka za kusongezwa kwa moto; mafuta yake pamoja na kidari atavileta, ili kwamba hicho kidari kitikiswe kuwa sadaka ya kutikiswa mbele za BWANA.

Tazama sura Nakili




Walawi 7:30
16 Marejeleo ya Msalaba  

Watu wako watajitoa kwa hiari, Siku ya uwezo wako; Kwa uzuri wa utakatifu, Tokea tumbo la asubuhi, Unao umande wa ujana wako.


Na kidari cha kutikiswa, na mguu wa kuinuliwa, mtavila katika mahali palipo safi; wewe, na wanao, na binti zako pamoja nawe; kwa maana vimetolewa kuwa ni haki yako, na haki ya wanao, katika zile kafara za sadaka za amani za wana wa Israeli.


Mguu wa kuinuliwa, na kidari cha kutikiswa, Watavileta pamoja na dhabihu zisongezwazo kwa njia ya moto, za hayo mafuta ili kuvitikisa viwe sadaka ya kutikiswa mbele za BWANA; kisha vitakuwa ni vyako wewe, na vya wanao pamoja nawe, ni haki yenu milele, kama BWANA alivyoagiza.


Naye atasongeza katika sadaka hiyo matoleo yake, dhabihu kwa BWANA kwa njia ya moto; yaani, mafuta yafunikayo matumbo, na mafuta yote yaliyo katika matumbo,


Naye atasongeza katika sadaka hiyo ya amani dhabihu kwa BWANA, itakayofanywa kwa njia ya moto; yaani, mafuta yake, na mkia wenye mafuta mzima, atauondoa kwa kuukata hapo karibu na mfupa wa maungoni; na mafuta yafunikayo matumbo, na mafuta yote yaliyo katika matumbo,


kisha akaweka vyote katika mikono ya Haruni, na katika mikono ya wanawe, na kuvitikisa huku na huko viwe sadaka ya kutikiswa mbele za BWANA.


Kisha Musa akakitwaa kile kidari, akakitikisa huku na huko, kiwe sadaka ya kutikiswa mbele za BWANA; ni sehemu ya Musa katika huyo kondoo dume wa kuwaweka wakfu; kama BWANA alivyomwagiza Musa.


nao wakayaweka hayo mafuta juu ya vidari, naye akayateketeza mafuta juu ya madhabahu;


na vile vidari, na mguu wa nyuma wa upande wa kulia, Haruni akavitikisa huku na huku viwe sadaka ya kutikiswa mbele ya BWANA; kama Musa alivyoagiza.


naye kuhani atavitikisa viwe sadaka ya kutikiswa mbele za BWANA; kitu hicho ni kitakatifu kwa kuhani, pamoja na kidari cha kutikiswa, na paja la kuinuliwa; kisha baadaye Mnadhiri ana ruhusa kunywa divai.


naye Haruni atawasongeza Walawi mbele za BWANA wawe sadaka ya kutikiswa, kwa ajili ya wana wa Israeli, ili wawe watumishi wa BWANA.


Hakuna mtu aniondoleaye, bali mimi nautoa mwenyewe. Nami ninao uweza wa kuutoa, ninao na uweza wa kuutwaa tena. Agizo hilo nililipokea kwa Baba yangu.


Maana, kama nia ipo, hukubaliwa kwa kadiri ya alivyo navyo mtu, si kwa kadiri ya asivyo navyo.


Na hii itakuwa haki ya makuhani kwa watu hao wasongezao sadaka, ikiwa ni ng'ombe au kondoo wampe kuhani mkono, na mashavu mawili, na tumbo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo