Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Walawi 7:14 - Swahili Revised Union Version

14 Na katika hayo atasongeza kimoja katika kila toleo kiwe sadaka ya kuinuliwa kwa BWANA; itakuwa ni ya kuhani atakayeinyunyiza hiyo damu ya sadaka za amani.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 Kutokana na maandazi hayo, atamtolea Mwenyezi-Mungu andazi moja kutoka kila sadaka; maandazi hayo yatakuwa yake kuhani anayeirashia madhabahu damu ya sadaka za amani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

14 Kutokana na maandazi hayo, atamtolea Mwenyezi-Mungu andazi moja kutoka kila sadaka; maandazi hayo yatakuwa yake kuhani anayeirashia madhabahu damu ya sadaka za amani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 Kutokana na maandazi hayo, atamtolea Mwenyezi-Mungu andazi moja kutoka kila sadaka; maandazi hayo yatakuwa yake kuhani anayeirashia madhabahu damu ya sadaka za amani.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 Ataleta moja ya kila aina ya andazi kuwa sadaka, matoleo kwa Mwenyezi Mungu; hii ni ya kuhani anayenyunyiza damu ya sadaka ya amani.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 Ataleta moja ya kila aina ya andazi kama sadaka, matoleo kwa bwana; hii ni ya kuhani anayenyunyiza damu ya sadaka ya amani.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

14 Na katika hayo atasongeza kimoja katika kila toleo kiwe sadaka ya kuinuliwa kwa BWANA; itakuwa ni ya kuhani atakayeinyunyiza hiyo damu ya sadaka za amani.

Tazama sura Nakili

Walawi 7:14
10 Marejeleo ya Msalaba  

Huyo kuhani atakayeisongeza kwa ajili ya dhambi ndiye atakayeila; italiwa katika mahali patakatifu, katika ua wa hema ya kukutania.

Sadaka zote za kuinuliwa za vitu vitakatifu, wana wa Israeli wavisongezavyo kwa BWANA, nimekupa wewe na wanao na binti zako pamoja nawe, ni haki yenu ya milele; ni agano la chumvi la milele mbele za BWANA kwa ajili yako, na kizazi chako pamoja nawe.

twaa katika nusu yao, ukampe Eleazari kuhani, kuwa sadaka ya kuinuliwa kwa BWANA.

Basi Musa akampa Eleazari kuhani hiyo sehemu, iliyokuwa sadaka ya kuinuliwa kwa BWANA, kama BWANA alivyomwagiza Musa.

Waangalieni hao Waisraeli walivyokuwa kwa jinsi ya mwili; wale wazilao dhabihu, je! Hawana shirika na madhabahu?

Wawe na fungu sawasawa la kula, pamoja na haya yaliyomfikia kwa kuuzwa urithi wa baba zake.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo