Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Walawi 6:9 - Swahili Revised Union Version

9 Haya, mwagize Haruni na wanawe, uwaambie, Amri ya sadaka ya kuteketezwa ni hii; hiyo sadaka ya kuteketezwa itakuwa pale motoni juu ya madhabahu usiku wote hadi asubuhi; na huo moto wa madhabahu utawaka juu yake usizimike.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 “Mpe Aroni na wanawe maagizo haya: Ufuatao ni mwongozo wa ibada kuhusu sadaka ya kuteketezwa. Sadaka ya kuteketezwa itakuwa motoni juu ya madhabahu usiku kucha hadi asubuhi na moto wake uchochewe, usizimike.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

9 “Mpe Aroni na wanawe maagizo haya: Ufuatao ni mwongozo wa ibada kuhusu sadaka ya kuteketezwa. Sadaka ya kuteketezwa itakuwa motoni juu ya madhabahu usiku kucha hadi asubuhi na moto wake uchochewe, usizimike.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 “Mpe Aroni na wanawe maagizo haya: ufuatao ni mwongozo wa ibada kuhusu sadaka ya kuteketezwa. Sadaka ya kuteketezwa itakuwa motoni juu ya madhabahu usiku kucha hadi asubuhi na moto wake uchochewe, usizimike.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 “Mpe Haruni na wanawe agizo hili: ‘Haya ndio masharti kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa: Sadaka ya kuteketezwa itabaki kwenye moto juu ya madhabahu usiku kucha, hadi asubuhi, nao moto lazima uwe unaendelea kuwaka juu ya madhabahu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

9 “Mpe Haruni na wanawe agizo hili: ‘Haya ndiyo masharti kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa: Sadaka ya kuteketezwa itabaki kwenye moto juu ya madhabahu usiku kucha, mpaka asubuhi, nao moto lazima uwe unaendelea kuwaka juu ya madhabahu.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

9 Haya, mwagize Haruni na wanawe, uwaambie, Amri ya sadaka ya kuteketezwa ni hii; hiyo sadaka ya kuteketezwa itakuwa pale motoni juu ya madhabahu usiku wote hadi asubuhi; na huo moto wa madhabahu utawaka juu yake usizimike.

Tazama sura Nakili




Walawi 6:9
10 Marejeleo ya Msalaba  

Na hicho kitakachosalia katika sadaka ya unga kitakuwa cha Haruni na wanawe; ni kitu kitakatifu sana katika sadaka zilizosongezwa kwa BWANA kwa njia ya moto.


na huo uliosalia wa ile sadaka ya unga utakuwa ni wa Haruni na wanawe; ni kitu kitakatifu sana katika sadaka zilizotolewa kwa BWANA kwa njia ya moto.


Nayo itakuwa ya Haruni na wanawe; nao wataila katika mahali patakatifu; kwa sababu kwake ni takatifu sana katika sadaka zitolewazo kwa BWANA kwa moto, kwa amri ya milele.


BWANA akanena na Musa, na kumwambia,


BWANA akanena na Musa na kumwambia,


Nawe utawaambia, Hii ndiyo sadaka isongezwayo kwa moto mtakayomsogezea BWANA; wana-kondoo dume wawili wa mwaka mmoja wakamilifu, kila siku, wawe sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote.


Tena katika siku ya Sabato watasongezwa wana-kondoo dume wawili, wa mwaka mmoja, wakamilifu, pamoja na sehemu ya mbili ya kumi za efa za unga laini kuwa sadaka ya unga, uliochanganywa na mafuta, pamoja na sadaka yake ya kinywaji;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo