Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Walawi 6:6 - Swahili Revised Union Version

6 Kisha ataleta sadaka yake ya hatia kwa BWANA, ni kondoo dume wa katika kundi lake, mkamilifu, sawasawa na hesabu utakayomwandikia, kuwa sadaka ya hatia, na kumpa kuhani;

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

6 Kisha atamletea kuhani kondoo dume au mbuzi dume asiye na dosari amtolee Mwenyezi-Mungu sadaka ya kuondoa hatia; thamani ya mnyama huyo itakuwa ile ya kawaida ya kuondoa hatia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

6 Kisha atamletea kuhani kondoo dume au mbuzi dume asiye na dosari amtolee Mwenyezi-Mungu sadaka ya kuondoa hatia; thamani ya mnyama huyo itakuwa ile ya kawaida ya kuondoa hatia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

6 Kisha atamletea kuhani kondoo dume au mbuzi dume asiye na dosari amtolee Mwenyezi-Mungu sadaka ya kuondoa hatia; thamani ya mnyama huyo itakuwa ile ya kawaida ya kuondoa hatia.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

6 Kisha kama adhabu lazima amletee kuhani, yaani kwa Mwenyezi Mungu, kuwa sadaka yake ya hatia, kondoo dume kutoka kundi lake asiye na dosari, mwenye thamani kamili.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

6 Kisha kama adhabu lazima amletee kuhani, yaani kwa bwana, kama sadaka yake ya hatia, kondoo dume asiye na dosari na mwenye thamani kamili kutoka kundi lake.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

6 Kisha ataleta sadaka yake ya hatia kwa BWANA, ni kondoo dume wa katika kundi lake, mkamilifu, sawasawa na hesabu utakayomwandikia, kuwa sadaka ya hatia, na kumpa kuhani;

Tazama sura Nakili

Walawi 6:6
8 Marejeleo ya Msalaba  

Nao wakatoa ahadi ya kwamba wataachana na wake zao; na kwa kuwa walikuwa na hatia, wakatoa kondoo dume kwa hatia yao.

tena kuleta malimbuko ya ardhi yetu, na malimbuko ya matunda yote ya miti ya namna zote, mwaka kwa mwaka, nyumbani kwa BWANA;

Nacho chumba kinachokabili upande wa kaskazini ni cha makuhani, wasimamizi wa madhabahu; hao ni wana wa Sadoki, ambao kati ya wana wa Lawi, ndio waliomkaribia BWANA, ili kumtumikia.

kisha kuhani atamshika mmoja kati ya hao wana-kondoo wa kiume, na kumsongeza awe sadaka ya hatia, pamoja na hiyo logi ya mafuta, kisha atavitikisa kuwa ni sadaka ya kutikiswa mbele za BWANA;

Mtu awaye yote akiasi na kufanya dhambi naye hakukusudia, katika mambo matakatifu ya BWANA; ndipo atakapomletea BWANA sadaka yake ya hatia, kondoo dume mkamilifu katika kundi lake; sawasawa na hesabu utakayomwandikia katika shekeli za fedha, kwa shekeli ya mahali patakatifu, kuwa sadaka ya hatia;

Naye ataleta kondoo dume wa kundi lake, mkamilifu, sawasawa na hesabu utakayomwandikia, kuwa sadaka ya hatia, amsongeze kwa huyo kuhani; na kuhani atamfanyia upatanisho kwa ajili ya jambo hilo alilolikosa pasipo kukusudia, asilijue, naye atasamehewa.

Lakini asipomweza mwana-kondoo, ndipo atakapomletea BWANA hua wawili, au makinda mawili ya njiwa, kuwa ni sadaka yake ya hatia ya jambo hilo alilolikosa; mmoja wa hao ndege kwa sadaka ya dhambi, na wa pili kwa sadaka ya kuteketezwa.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo