Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Walawi 6:27 - Swahili Revised Union Version

27 Kila kitu kitakachoigusa nyama ya sadaka hiyo kitakuwa kitakatifu; tena itakapomwagika damu yake yeyote katika nguo yoyote, utaifua nguo hiyo iliyomwagiwa, katika mahali patakatifu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

27 Chochote kitakachogusa nyama hiyo kitakuwa kitakatifu; vazi lolote likidondokewa na damu ya sadaka hiyo, basi, vazi hilo litaoshewa mahali patakatifu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

27 Chochote kitakachogusa nyama hiyo kitakuwa kitakatifu; vazi lolote likidondokewa na damu ya sadaka hiyo, basi, vazi hilo litaoshewa mahali patakatifu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

27 Chochote kitakachogusa nyama hiyo kitakuwa kitakatifu; vazi lolote likidondokewa na damu ya sadaka hiyo, basi, vazi hilo litaoshewa mahali patakatifu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

27 Chochote kitakachogusa nyama yoyote ya hiyo sadaka kitakuwa kitakatifu; na kama damu ya hiyo sadaka itadondokea juu ya vazi, lazima ulifulie mahali patakatifu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

27 Chochote kitakachogusa nyama yoyote ya hiyo sadaka kitakuwa kitakatifu, na kama hiyo damu itadondokea juu ya vazi, lazima uifulie mahali patakatifu.

Tazama sura Nakili




Walawi 6:27
11 Marejeleo ya Msalaba  

Utafanya upatanisho kwa ajili ya hiyo madhabahu muda wa siku saba, na kuitakasa; ndipo madhabahu itakapokuwa takatifu sana; kila kitu kiigusacho madhabahu kitakuwa kitakatifu.


Nawe utavitakasa vitu hivyo, ili viwe vitakatifu sana; tena kila kivigusacho vyombo vile kitakuwa kitakatifu.


Nao watakapotoka kuingia ua wa nje, yaani, ua wa nje wa watu, ndipo watakapoyavua mavazi yao waliyovaa katika huduma yao, na kuyaweka katika vile vyumba vitakatifu, nao watavaa mavazi mengine, wasije wakawatakasa watu kwa mavazi yao.


Tena kitu chochote, wanyama hao mmojawapo atakachokiangukia, wakiisha kufa, kitakuwa ni najisi; cha mti, nguo, ngozi, gunia, chombo chochote cha kufanyia kazi yoyote, lazima kitiwe ndani ya maji, nacho kitakuwa ni najisi hadi jioni; ndipo kitakapokuwa ni safi.


Kila mwanamume miongoni mwa wana wa Haruni atakula katika huo, kuwa ni haki yao milele katika vizazi vyenu, katika matoleo ya BWANA yasongezwayo kwa njia ya moto; mtu yeyote atakayevigusa atakuwa ni mtakatifu.


Tena nyama itakayogusa kitu kilicho najisi haitaliwa; itachomwa moto. Na katika hiyo nyama nyingine, kila mtu aliye safi ana ruhusa kuila;


Mtu akichukua nyama takatifu katika upindo wa nguo yake, naye kwa upindo wake akagusa mkate, au ugali, au divai, au mafuta, au chakula chochote, je, Kitu hicho kitakuwa kitakatifu? Makuhani wakajibu, wakasema, La.


nao wakamsihi waguse hata pindo la vazi lake tu; na wote waliogusa wakaponywa kabisa.


Kwa maana alisema moyoni mwake, Nikigusa tu upindo wa vazi lake nitapona.


Basi, wapenzi wangu, kwa kuwa tuna ahadi hizo, na tujitakase nafsi zetu kutoka kwa uchafu wote wa mwili na roho, huku tukitimiza utakatifu katika kumcha Mungu.


Maana, angalieni, kuhuzunishwa kuko huko kwa jinsi ya Mungu kulitenda bidii gani ndani yenu; naam, na kujitetea, naam, na kukasirika, naam, na hofu, naam, na shauku, naam, na kujitahidi, naam, na kisasi! Kwa kila njia mmejionesha wenyewe kuwa safi katika jambo hilo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo