Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Walawi 5:2 - Swahili Revised Union Version

2 au kama mtu akigusa kitu kilicho najisi, iwe ni mzoga wa mnyama nyikani aliye najisi, au ni mzoga wa mnyama wa mfugo aliye najisi, au ni mzoga wa mdudu aliye najisi, bila kujua, akapata kuwa najisi, ndipo atakapochukua uovu wake;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 Au kama mtu yeyote miongoni mwenu amekuwa najisi bila kukusudia kwa kugusa kitu chochote najisi, iwe ni mzoga wa mnyama wa porini au wa kufugwa au wadudu, atakuwa na hatia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

2 Au kama mtu yeyote miongoni mwenu amekuwa najisi bila kukusudia kwa kugusa kitu chochote najisi, iwe ni mzoga wa mnyama wa porini au wa kufugwa au wadudu, atakuwa na hatia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 Au kama mtu yeyote miongoni mwenu amekuwa najisi bila kukusudia kwa kugusa kitu chochote najisi, iwe ni mzoga wa mnyama wa porini au wa kufugwa au wadudu, atakuwa na hatia.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 “ ‘Au mtu akitambua kuwa ana hatia, kama vile akigusa kitu chochote ambacho ni najisi, iwe ni mizoga ya wanyama pori walio najisi, au ya wanyama wafugwao walio najisi, au ya viumbe vinavyotambaa ardhini, hata akiwa hana habari, amekuwa najisi na mwenye hatia.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 “ ‘Au kama mtu akigusa kitu chochote ambacho ni najisi, iwe ni mizoga ya wanyama pori walio najisi, au ya wanyama wafugwao walio najisi, au ya viumbe vitambaavyo ardhini, hata akiwa hana habari, amekuwa najisi na mwenye hatia.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

2 au kama mtu akigusa kitu kilicho najisi, iwe ni mzoga wa mnyama nyikani aliye najisi, au ni mzoga wa mnyama afugwae aliye najisi, au ni mzoga wa mdudu aliye najisi, bila kujua, akapata kuwa najisi, ndipo atakapochukua uovu wake;

Tazama sura Nakili




Walawi 5:2
16 Marejeleo ya Msalaba  

Ni nani awezaye kuyatambua makosa yake? Unitakase na mambo ya siri.


Nendeni zenu, nendeni zenu, tokeni huko, msiguse kitu kichafu; tokeni kati yake; iweni safi ninyi mnaochukua vyombo vya BWANA.


watakuwa machukizo kwenu; msiile nyama yao, na mizoga yao itakuwa machukizo kwenu.


Msiile nyama yao, wala msiiguse mizoga yao; hao ni najisi kwenu.


Na kama mkutano mzima wa Israeli ukifanya dhambi bila kukusudia, na jambo lenyewe likayafichamania macho ya huo mkutano, nao wamefanya mojawapo katika mambo yaliyozuiliwa na BWANA, kwamba wasiyafanye, nao wamepata hatia;


Na kama mtu akifanya dhambi, na kutenda mambo hayo mojawapo ambayo BWANA alizuilia yasifanywe, ajapokuwa hakuyajua, ni mwenye hatia pia, naye atachukua uovu wake.


au kama akiugusa uchafu wa binadamu, uchafu wowote ambao kwao amepata unajisi, bila kujua, hapo apatapo kulijua, ndipo atakapokuwa na hatia;


au, kama mtu akijiapisha, kwa kutamka haraka kwa midomo yake, kutenda uovu, au kutenda mema, neno lolote mtu atakalolitamka kwa kiapo pasipo kufikiri, bila kujua; hapo atakapolijua, ndipo atakapokuwa na hatia katika mambo hayo mojawapo;


Kisha mtu awaye yote atakapogusa kitu chochote kilicho najisi, uchafu wa binadamu, au mnyama aliye najisi, au machukizo yoyote yaliyo najisi, kisha akala nyama ya dhabihu ya sadaka za amani, ambazo ni za BWANA, mtu huyo atakatiliwa mbali na watu wake.


Ndipo Hagai akasema, Kama mtu aliyetiwa unajisi kwa kugusa maiti, akigusa kimojawapo cha vitu hivi, je, Kitakuwa najisi? Makuhani wakajibu, wakasema, Kitakuwa najisi.


Na kitu chochote atakachokigusa mtu aliye najisi kitakuwa najisi; na mtu atakayekigusa kitu hicho atakuwa najisi hadi jioni.


Ole wenu, kwa kuwa mmefanana na makaburi yasiyoonekana, ambayo watu wapitao juu yake hawana habari nayo.


Kwa hiyo, Tokeni kati yao, Mkatengwe nao, asema Bwana, Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha.


na nguruwe, kwa kuwa amepasuliwa ukwato lakini hacheui, huyu ni najisi kwenu msile nyama zao, wala mizoga yao msiiguse.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo