Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Walawi 3:16 - Swahili Revised Union Version

16 Naye kuhani atayateketeza kwa moto juu ya madhabahu; ni chakula cha dhabihu ya kusongezwa kwa njia ya moto, iwe harufu ya kupendeza; mafuta yote ni ya BWANA.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 Kuhani ataviteketeza juu ya madhabahu kama chakula kinachotolewa kwa Mwenyezi-Mungu kwa moto kutoa harufu ya kumpendeza Mungu. Mafuta yote ni ya Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 Kuhani ataviteketeza juu ya madhabahu kama chakula kinachotolewa kwa Mwenyezi-Mungu kwa moto kutoa harufu ya kumpendeza Mungu. Mafuta yote ni ya Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 Kuhani ataviteketeza juu ya madhabahu kama chakula kinachotolewa kwa Mwenyezi-Mungu kwa moto kutoa harufu ya kumpendeza Mungu. Mafuta yote ni ya Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 Kuhani ataviteketeza juu ya madhabahu viwe chakula, sadaka iliyotolewa kwa moto, harufu nzuri. Mafuta yote ya mnyama ni ya Mwenyezi Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 Kuhani ataviteketeza juu ya madhabahu kama chakula, sadaka iliyotolewa kwa moto, harufu nzuri. Mafuta yote ya mnyama ni ya bwana.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

16 Naye kuhani atayateketeza kwa moto juu ya madhabahu; ni chakula cha dhabihu ya kusongezwa kwa njia ya moto, iwe harufu ya kupendeza; mafuta yote ni ya BWANA.

Tazama sura Nakili




Walawi 3:16
19 Marejeleo ya Msalaba  

Habili naye akaleta wazao wa kwanza wa wanyama wake na sehemu zilizonona za wanyama. BWANA akamtakabali Habili na sadaka yake;


Na tena sadaka za kuteketezwa nazo zilikuwa nyingi, pamoja na mafuta ya sadaka za amani, na sadaka za kinywaji kwa kila sadaka ya kuteketezwa. Hivyo ikatengezeka huduma ya nyumba ya BWANA.


Tena Sulemani akaitakasa behewa katikati, iliyokuwa mbele ya nyumba ya BWANA; kwa kuwa hapo ndipo alipotoa sadaka za kuteketezwa, na mafuta ya sadaka za amani; kwa sababu ile madhabahu ya shaba aliyoifanya Sulemani haikutosha kuzipokea sadaka za kuteketezwa, na sadaka za unga, na mafuta.


Kisha twaa mafuta yote yafunikayo matumbo, na kitambi kilicho katika ini, na figo mbili, na mafuta yaliyo juu yake, uyateketeze yote juu ya madhabahu.


Tena yatwae mafuta ya huyo kondoo dume, na mkia wake wa mafuta, na mafuta yafunikayo matumbo, na kitambi kilicho katika ini, na figo mbili, na mafuta yaliyo katika hizo figo, na paja la kulia; kwani ni kondoo ambaye ni wa kuwekwa kwa kazi takatifu;


Lakini BWANA aliridhika kumchubua; Amemhuzunisha; Utakapofanya nafsi yake kuwa dhabihu kwa dhambi, Ataona uzao wake, ataishi siku nyingi, Na mapenzi ya BWANA yatafanikiwa mkononi mwake;


Lakini makuhani Walawi, wana wa Sadoki, waliosimamia patakatifu pangu, hapo wana wa Israeli walipopotea na kuniacha, hao ndio watakaonikaribia ili kunihudumia; nao watasimama mbele zangu, kunitolea mafuta na damu, asema Bwana MUNGU;


Naye kuhani atainyunyiza damu yake juu ya madhabahu ya BWANA, mlangoni pa hema ya kukutania, na kuyateketeza mafuta yake, yawe harufu njema mbele za BWANA.


Na mafuta yake yote atayateketeza juu ya madhabahu, kama alivyoyateketeza mafuta ya hizo sadaka za amani; naye kuhani atamfanyia upatanisho kwa ajili ya dhambi yake, naye atasamehewa.


Kisha atayaondoa mafuta yake yote, kama vile mafuta yanavyoondolewa katika hizo sadaka za amani; kisha kuhani atayateketeza juu ya madhabahu, iwe harufu ya kupendeza kwa BWANA; na kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake, naye atasamehewa.


Kisha akayatwaa hayo mafuta, na mkia wenye mafuta, na mafuta yote yaliyokuwa katika matumbo, na kitambi cha ini, na figo mbili, na mafuta yake, na mguu wa nyuma wa upande wa kulia;


Kisha moto ukatoka hapo mbele za BWANA, na kuiteketeza sadaka ya kuteketezwa, na yale mafuta juu ya madhabahu; watu wote walipouona huo moto wakapiga kelele wakainama kifudifudi.


Akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo