Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Walawi 23:11 - Swahili Revised Union Version

11 naye atautikisa mganda mbele za BWANA ili kwamba ukubaliwe kwa ajili yenu; siku ya pili baada ya Sabato kuhani atautikisa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 Kuhani atafanya nayo ishara ya kunitolea siku inayofuata siku ya Sabato ili mpate kukubaliwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 Kuhani atafanya nayo ishara ya kunitolea siku inayofuata siku ya Sabato ili mpate kukubaliwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 Kuhani atafanya nayo ishara ya kunitolea siku inayofuata siku ya Sabato ili mpate kukubaliwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 Naye atauinua huo mganda mbele za Mwenyezi Mungu ili ukubaliwe kwa niaba yenu; kuhani ataupunga siku inayofuata Sabato.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 Naye atauinua huo mganda mbele za bwana ili ukubaliwe kwa niaba yenu; kuhani ataupunga siku inayofuata Sabato.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

11 naye atautikisa mganda mbele za BWANA ili kwamba ukubaliwe kwa ajili yenu; siku ya pili baada ya Sabato kuhani atautikisa.

Tazama sura Nakili




Walawi 23:11
7 Marejeleo ya Msalaba  

Nalo litakuwa katika kipaji cha uso cha Haruni, na Haruni atauchukua uovu wa vile vitu vitakatifu, watakavyovitakasa hao wana wa Israeli katika vipawa vyao vyote vitakatifu, nalo litakuwa katika kipaji chake cha uso sikuzote, ili vipate kukubaliwa mbele za BWANA.


nawe utavitia hivi vyote katika mikono ya Haruni, na katika mikono ya wanawe; nawe utavitikisatikisa viwe sadaka ya kutikiswa mbele za BWANA.


Na kidari cha kutikiswa, na mguu wa kuinuliwa, mtavila katika mahali palipo safi; wewe, na wanao, na binti zako pamoja nawe; kwa maana vimetolewa kuwa ni haki yako, na haki ya wanao, katika zile kafara za sadaka za amani za wana wa Israeli.


Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Hapo mtakapoingia katika hiyo nchi niwapayo, na kuyavuna mavuno yake, ndipo mtakapomletea kuhani mganda wa malimbuko ya mavuno yenu;


Na siku hiyo mtakayoutikisa mganda, mtamsongeza mwana-kondoo wa kiume asiye na dosari wa mwaka wa kwanza, awe sadaka ya kuteketezwa kwa BWANA.


na vile vidari, na mguu wa nyuma wa upande wa kulia, Haruni akavitikisa huku na huku viwe sadaka ya kutikiswa mbele ya BWANA; kama Musa alivyoagiza.


Basi Naomi akarudi; pamoja na Ruthu Mmoabi, mkwewe; ambao walirudi kutoka nchi ya Moabu; nao wakafika Bethlehemu mwanzo wa mavuno ya shayiri.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo