Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Walawi 22:4 - Swahili Revised Union Version

4 Mtu yeyote wa kizazi cha Haruni aliye na ukoma, au kisonono; asile katika vitu vitakatifu, hata atakapokuwa safi. Tena mtu yeyote atakayekinusa kitu kilicho na unajisi kwa sababu ya wafu, au mtu ambaye shahawa humtoka;

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 Mtu yeyote wa nasaba ya Aroni akiwa na ugonjwa wa ukoma au anatokwa usaha asile vitu vitakatifu mpaka atakapokuwa safi. Mtu yeyote akimgusa mtu aliyetiwa unajisi kwa kugusa maiti au mtu aliyetokwa na shahawa,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 Mtu yeyote wa nasaba ya Aroni akiwa na ugonjwa wa ukoma au anatokwa usaha asile vitu vitakatifu mpaka atakapokuwa safi. Mtu yeyote akimgusa mtu aliyetiwa unajisi kwa kugusa maiti au mtu aliyetokwa na shahawa,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 Mtu yeyote wa nasaba ya Aroni akiwa na ugonjwa wa ukoma au anatokwa usaha asile vitu vitakatifu mpaka atakapokuwa safi. Mtu yeyote akimgusa mtu aliyetiwa unajisi kwa kugusa maiti au mtu aliyetokwa na shahawa,

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 “ ‘Ikiwa mzao wa Haruni ana ugonjwa wa ngozi unaoambukiza au anatokwa na usaha mwilini, hawezi kula sadaka takatifu hadi atakasike. Pia atakuwa najisi akigusa kitu chochote kilicho najisi kutokana na kugusa maiti, au akigusa mtu aliyetokwa na shahawa,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 “ ‘Ikiwa mzao wa Haruni ana ugonjwa wa ngozi unaoambukiza au anatokwa na usaha mwilini, hawezi kula sadaka takatifu mpaka atakasike. Pia atakuwa najisi ikiwa atagusa kitu chochote kilicho najisi kwa kugusa maiti au mtu aliyetokwa na shahawa,

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

4 Mtu yeyote wa kizazi cha Haruni aliye na ukoma, au kisonono; asile katika vitu vitakatifu, hata atakapokuwa safi. Tena mtu yeyote atakayekinusa kitu kilicho na unajisi kwa sababu ya wafu, au mtu ambaye shahawa humtoka;

Tazama sura Nakili

Walawi 22:4
18 Marejeleo ya Msalaba  

Mnyama yeyote ambaye mna ruhusa kumla akifa, yeye anayeugusa mzoga wake atakuwa najisi hadi jioni.

Na kila nguo au ngozi, ambayo ina shahawa, itafuliwa kwa maji, nayo itakuwa najisi hata jioni.

Na hicho kitakachosalia katika sadaka ya unga kitakuwa cha Haruni na wanawe; ni kitu kitakatifu sana katika sadaka zilizosongezwa kwa BWANA kwa njia ya moto.

na huo uliosalia wa ile sadaka ya unga utakuwa ni wa Haruni na wanawe; ni kitu kitakatifu sana katika sadaka zilizotolewa kwa BWANA kwa njia ya moto.

Kisha BWANA akamwambia Musa, Nena na hao makuhani, wana wa Haruni, uwaambie, Mtu asijinajisi kwa ajili ya wafu katika watu wake;

Atakula chakula cha Mungu wake, katika hicho kilicho kitakatifu sana, na hicho kilicho kitakatifu.

Ndipo Hagai akasema, Kama mtu aliyetiwa unajisi kwa kugusa maiti, akigusa kimojawapo cha vitu hivi, je, Kitakuwa najisi? Makuhani wakajibu, wakasema, Kitakuwa najisi.

Sadaka zote za kuinuliwa za vitu vitakatifu, wana wa Israeli wavisongezavyo kwa BWANA, nimekupa wewe na wanao na binti zako pamoja nawe, ni haki yenu ya milele; ni agano la chumvi la milele mbele za BWANA kwa ajili yako, na kizazi chako pamoja nawe.

Vitu hivi vitakuwa vyako katika vile vilivyo vitakatifu sana, visiteketezwe motoni; matoleo yao yote, maana, kila sadaka yao ya unga, na kila sadaka yao ya dhambi, na kila sadaka yao ya hatia watakayonitolea, vitakuwa vitakatifu sana kwa ajili yako wewe na kwa wanao.

Lakini mtu atakayekuwa najisi, naye hataki kujitakasa, mtu huyo atakatiliwa mbali katika mkutano, kwa sababu amepatia unajisi mahali patakatifu pa BWANA; hayo maji ya farakano hayakunyunyizwa juu yake; yeye yuko najisi.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo