Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Walawi 22:19 - Swahili Revised Union Version

19 ili mpate kukubaliwa, mtaleta dume mkamilifu, katika ng'ombe, au katika kondoo, au katika mbuzi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

19 ili apate kukubalika, atatoa katika ng'ombe dume au katika kondoo dume asiye na dosari.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

19 ili apate kukubalika, atatoa katika ng'ombe dume au katika kondoo dume asiye na dosari.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

19 ili apate kukubalika, atatoa katika ng'ombe dume au katika kondoo dume asiye na dosari.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

19 lazima amtoe mnyama dume asiye na dosari, akiwa ng’ombe, mbuzi au kondoo, ili aweze kukubalika kwa niaba yako.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

19 lazima mtoe mnyama dume asiye na dosari, akiwa ng’ombe, mbuzi au kondoo, ili aweze kukubalika kwa niaba yako.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

19 ili mpate kukubaliwa, mtaleta dume mkamilifu, katika ng'ombe, au katika kondoo, au katika mbuzi.

Tazama sura Nakili




Walawi 22:19
21 Marejeleo ya Msalaba  

Mwana-kondoo wenu atakuwa hana dosari, wa kiume wa mwaka mmoja; mtamtwaa katika kondoo au katika mbuzi.


Na matoleo yake kwamba ni katika kundi, katika kondoo, au katika mbuzi, kuwa sadaka ya kuteketezwa; atatoa dume asiye na dosari.


Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Mtu wa kwenu atakapomtolea BWANA matoleo, mtatoa matoleo yenu katika wanyama wa kufugwa, katika ng'ombe, kondoo na mbuzi.


Ikawa matoleo yake ni sadaka ya kuteketezwa ya ng'ombe, atatoa ng'ombe dume mkamilifu; ataleta mlangoni pa hema ya kukutania, ili akubaliwe mbele ya BWANA.


Kwa kuwa mtu aliye na kasoro ya kimwili hatakaribia, asiyeoana, aliyelemaa mguu au mtu aliyejeruhika uso, au kiungo kilichozidi vimpasavyo mwili,


Naye akileta mwana-kondoo kuwa sadaka ya dhambi, ataleta wa kike mkamilifu.


Na alipokuwa ameketi juu ya kiti cha hukumu, mkewe alimpelekea mjumbe, kumwambia, Usiwe na neno na yule mwenye haki; kwa sababu nimeteswa mengi leo katika ndoto kwa ajili yake.


Basi Pilato alipoona ya kuwa hafai lolote, bali ghasia inazidi tu, akatwaa maji, akanawa mikono yake mbele ya mkutano, akasema, Mimi sina hatia katika damu ya mtu huyu mwenye haki; yaangalieni haya ninyi wenyewe.


Wakasema, Basi, haya yatuhusu nini sisi? Yaangalie haya wewe mwenyewe.


Basi yule afisa, na hao waliokuwa pamoja naye wakimlinda Yesu, walipoliona tetemeko la ardhi na mambo yaliyofanyika, wakaogopa sana, wakisema, Hakika huyu alikuwa Mwana wa Mungu.


akawaambia, Mtu huyu mmemleta kwangu kana kwamba anapotosha watu; nami, tazama, nimeamua mambo yake mbele yenu, ila sikuona kwake kosa lolote katika mambo hayo mliyomshitaki;


Nayo ni haki kwetu sisi, kwa kuwa tunapokea malipo tuliyostahili kwa matendo yetu; bali huyu hakutenda lolote lisilofaa.


Alipokwisha kusema hayo alikata roho. Yule jemadari alipoona yaliyotukia, alimtukuza Mungu, akisema, Hakika yake, mtu huyu alikuwa mwenye haki.


Kisha Pilato akatokea tena nje, akawaambia, Mtu huyu namleta nje kwenu, mpate kufahamu ya kuwa mimi sioni hatia yoyote kwake.


Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika Yeye.


apate kujiletea kanisa tukufu, lisilo na dosari wala kunyanzi wala lolote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa.


Lakini akiwa na kilema, akichechea, au akiwa kipofu, au mwenye kilema kibaya chochote, usimsongezee BWANA, Mungu wako, sadaka.


basi si zaidi damu yake Kristo, ambaye kwamba kwa Roho wa milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo na dosari, itawasafisha dhamiri zenu na matendo mafu, mpate kumwabudu Mungu aliye hai?


bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana-kondoo asiye na dosari wala waa, yaani, ya Kristo.


Kwa maana Kristo naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio haki, ili atulete kwa Mungu; akauawa kimwili, lakini akahuishwa kiroho,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo