Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Walawi 19:5 - Swahili Revised Union Version

5 Nanyi hapo mtakapomchinjia BWANA sadaka ya amani mtaitoa kwa njia ipasayo ili mpate kukubaliwa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 “Mnaponitolea mimi Mwenyezi-Mungu sadaka za amani, mtanitolea kama itakiwavyo ili mpate kukubaliwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

5 “Mnaponitolea mimi Mwenyezi-Mungu sadaka za amani, mtanitolea kama itakiwavyo ili mpate kukubaliwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 “Mnaponitolea mimi Mwenyezi-Mungu sadaka za amani, mtanitolea kama itakiwavyo ili mpate kukubaliwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 “ ‘Mnapotoa dhabihu ya sadaka ya amani kwa Mwenyezi Mungu, toeni kwa namna ambayo itakubaliwa kwa niaba yenu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 “ ‘Mnapotoa dhabihu ya sadaka ya amani kwa bwana, toeni kwa namna ambayo itakubaliwa kwa niaba yenu.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

5 Nanyi hapo mtakapomchinjia BWANA sadaka ya amani mtaitoa kwa njia ipasayo ili mpate kukubaliwa.

Tazama sura Nakili




Walawi 19:5
16 Marejeleo ya Msalaba  

Hezekia akaziweka zamu za makuhani na Walawi kwa zamu zao, kila mtu kwa kadiri ya huduma yake, makuhani na Walawi pia, kwa sadaka za kuteketezwa na kwa sadaka za amani, kutumika, na kushukuru, na kusifu, malangoni mwa kambi ya BWANA.


akapeleka vijana wa wana wa Israeli, waliotoa sadaka za kuteketezwa, wakamchinjia BWANA sadaka za amani za ng'ombe.


Naye mkuu atakapotengeneza sadaka atoayo kwa hiari yake mwenyewe, sadaka ya kuteketezwa, au sadaka za amani, ziwe sadaka amtoleazo BWANA kwa hiari yake mwenyewe, mtu mmoja atamfungulia lango lile lielekealo upande wa mashariki, naye ataitoa sadaka yake ya kuteketezwa, na sadaka zake za amani, kama afanyavyo siku ya sabato; kisha atatoka; na baada ya kutoka kwake mtu mmoja atalifunga lango.


Naye mkuu ataingia kwa njia ya ukumbi wa lango lile, upande wa nje, naye atasimama karibu na mwimo wa lango, nao makuhani wataitengeneza sadaka yake ya kuteketezwa, na sadaka zake za amani, naye ataabudu penye kizingiti cha lango; kisha atatoka; lakini lango lile halitafungwa hadi wakati wa jioni.


Ikawa matoleo yake ni sadaka ya kuteketezwa ya ng'ombe, atatoa ng'ombe dume mkamilifu; ataleta mlangoni pa hema ya kukutania, ili akubaliwe mbele ya BWANA.


Msigeuke kufuata sanamu, wala msijitengenezee miungu ya kusubu mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.


Italiwa siku iyo hiyo mliyoichinja, na siku ya pili yake; na kama kitu chochote katika sadaka hiyo kilisalia hata siku ya tatu kitachomwa moto.


ili mpate kukubaliwa, mtaleta dume mkamilifu, katika ng'ombe, au katika kondoo, au katika mbuzi.


Na mtu yeyote atakayemtolea BWANA dhabihu katika sadaka za amani, ili kuondoa nadhiri, au sadaka ya moyo wa kupenda, katika ng'ombe, au katika kondoo, atakuwa mkamilifu, apate kukubaliwa; pasiwe na kilema chochote ndani yake.


Ng'ombe, au mwana-kondoo aliye na kitu kilichozidi, au aliyepungukiwa na kitu katika vitu vya mwilini mwake, mna ruhusa kutoa kuwa sadaka ya moyo wa kupenda; lakini kwa ajili ya nadhiri hatakubaliwa.


Tena mtakapomchinjia BWANA dhabihu ya shukrani, mtamchinja ili mpate kukubaliwa.


Lakini ikiwa hii sadaka ya matoleo yake ni nadhiri, au sadaka ya hiari, italiwa siku hiyo aliyoileta sadaka yake; kisha siku ya pili yake kitakachosalia kitaliwa;


Tena kama nyama yoyote katika hiyo dhabihu yake ya sadaka za amani ikiliwa siku ya tatu, haitakubaliwa, wala haitahesabiwa kwake huyo mwenye kuisongeza; itakuwa ni machukizo, na mtu atakayeila atachukua uovu wake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo