Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Walawi 19:22 - Swahili Revised Union Version

22 Kisha huyo kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake, kwa huyo kondoo dume wa sadaka ya hatia mbele za BWANA, kwa ajili ya dhambi yake aliyoifanya; naye atasamehewa hiyo dhambi yake aliyoifanya.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

22 Kuhani atamfanyia ibada ya upatanisho kwa kutumia kondoo huyo mbele ya Mwenyezi-Mungu kwa ajili ya dhambi aliyotenda; naye atasamehewa dhambi hiyo aliyotenda.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

22 Kuhani atamfanyia ibada ya upatanisho kwa kutumia kondoo huyo mbele ya Mwenyezi-Mungu kwa ajili ya dhambi aliyotenda; naye atasamehewa dhambi hiyo aliyotenda.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

22 Kuhani atamfanyia ibada ya upatanisho kwa kutumia kondoo huyo mbele ya Mwenyezi-Mungu kwa ajili ya dhambi aliyotenda; naye atasamehewa dhambi hiyo aliyotenda.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

22 Kupitia kwa huyo kondoo dume wa sadaka ya hatia, kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake mbele za Mwenyezi Mungu kwa ajili ya dhambi aliyotenda, naye atasamehewa dhambi yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

22 Kupitia kwa huyo kondoo dume wa sadaka ya hatia, kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake mbele za bwana kwa ajili ya dhambi aliyotenda, naye atasamehewa dhambi yake.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

22 Kisha huyo kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake, kwa huyo kondoo dume wa sadaka ya hatia mbele za BWANA, kwa ajili ya dhambi yake aliyoifanya; naye atasamehewa hiyo dhambi yake aliyoifanya.

Tazama sura Nakili

Walawi 19:22
7 Marejeleo ya Msalaba  

Na huyo mwanamume ataleta sadaka yake ya hatia aitoe kwa BWANA, hata mlangoni pa hema ya kukutania; kondoo dume kwa hiyo sadaka ya hatia.

Nanyi mtakapoingia katika nchi ile, na kupanda miti ya namna zote kwa ajili ya chakula, ndipo mtayahesabu matunda yake kama yaliyotakazwa; kwa muda wa miaka mitatu miti hiyo itakuwa kwenu kama katazo; matunda yake hayataliwa.

Ndivyo atakavyomfanyia huyo ng'ombe; kama alivyomfanyia huyo ng'ombe wa sadaka ya dhambi, atamfanyia na huyu hivyo; naye kuhani atawafanyia upatanisho, nao watasamehewa.

Na mafuta yake yote atayateketeza juu ya madhabahu, kama alivyoyateketeza mafuta ya hizo sadaka za amani; naye kuhani atamfanyia upatanisho kwa ajili ya dhambi yake, naye atasamehewa.

Kisha atayaondoa mafuta yake yote, kama vile mafuta yanavyoondolewa katika hizo sadaka za amani; kisha kuhani atayateketeza juu ya madhabahu, iwe harufu ya kupendeza kwa BWANA; na kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake, naye atasamehewa.

kisha atayaondoa mafuta yake yote, kama mafuta ya mwana-kondoo yalivyoondolewa katika hizo sadaka za amani; kisha kuhani atayateketeza juu ya madhabahu, kwa desturi ya hizo sadaka za BWANA zilizosongezwa kwa njia ya moto; na kuhani atamfanyia upatanisho kwa ajili ya hiyo dhambi yake aliyoifanya, naye atasamehewa.

Lakini asipomweza mwana-kondoo, ndipo atakapomletea BWANA hua wawili, au makinda mawili ya njiwa, kuwa ni sadaka yake ya hatia ya jambo hilo alilolikosa; mmoja wa hao ndege kwa sadaka ya dhambi, na wa pili kwa sadaka ya kuteketezwa.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo