Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Walawi 18:30 - Swahili Revised Union Version

30 Kwa hiyo yafuateni maagizo yangu, ili kamwe msiwe na mojawapo ya tabia hizi zinazochukiza, zilizotangulia kufanywa mbele zenu; mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

30 Kwa hiyo shikeni kikamilifu yote ninayowaagiza; msifuate mazoea yoyote ya kuchukiza yaliyofanywa na wale walioishi nchini kabla yenu, msije mkajitia unajisi kwayo. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

30 Kwa hiyo shikeni kikamilifu yote ninayowaagiza; msifuate mazoea yoyote ya kuchukiza yaliyofanywa na wale walioishi nchini kabla yenu, msije mkajitia unajisi kwayo. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

30 Kwa hiyo shikeni kikamilifu yote ninayowaagiza; msifuate mazoea yoyote ya kuchukiza yaliyofanywa na wale walioishi nchini kabla yenu, msije mkajitia unajisi kwayo. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

30 Shikeni maagizo yangu, wala msifuate desturi za machukizo yoyote yaliyofanywa kabla hamjafika katika nchi hii, na kujitia unajisi kwa hayo. Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, Mungu wenu.’ ”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

30 Shikeni maagizo yangu, wala msifuate desturi za machukizo yoyote yaliyofanywa kabla hamjafika katika nchi hii, na kujitia unajisi kwa hayo. Mimi ndimi bwana Mwenyezi Mungu wako.’ ”

Tazama sura Nakili




Walawi 18:30
14 Marejeleo ya Msalaba  

Na mahanithi walikuwako katika nchi, wakafanya sawasawa na machukizo yote ya mataifa BWANA aliowafukuza mbele ya wana wa Israeli.


Akachukiza mno, kwa kuzifuata sanamu sawasawa na yote waliyoyafanya Waamori, BWANA aliowafukuza mbele ya wana wa Israeli.)


Na mambo hayo yalipotendeka, wakuu wakanikaribia, wakisema, Watu wa Israeli, na makuhani, na Walawi, hawakujitenga na watu wa nchi hizi, na machukizo yao, yaani, ya Wakanaani, na Wahiti, na Waperizi, na Wayebusi, na Waamoni, na Wamoabi, na Wamisri, na Waamori.


Kwani mtu yeyote atakayefanya mojawapo ya machukizo hayo, nafsi hizo zitakazoyafanya zitakatiliwa mbali na watu wao.


BWANA akanena na Musa, akamwambia,


Nanyi msiende kwa kuzifuata desturi za taifa, niitoayo mbele yenu; kwa kuwa wao waliyafanya mambo hayo yote, na kwa ajili ya hayo niliwachukia.


Basi kwa hiyo watayashika maagizo yangu, wasije wakachukua dhambi kwa hayo, nao wakafa humo, wakiyanajisi; mimi ndimi BWANA niwatakasaye.


Kwa ajili hii mpende BWANA, Mungu wako, na kushika sikuzote mausia yake, na amri zake, na hukumu zake, na maagizo yake.


ujiangalie, usije ukanaswa ukawafuata, wakiisha kuangamizwa mbele yako; wala usije ukauliza habari za miungu yao, ukisema, Mataifa haya waitumikiaje miungu yao? Nami nifanye hivyo.


Usimtende kama haya BWANA, Mungu wako; kwani kila yaliyo machukizo kwa BWANA, ayachukiayo yeye, wameifanyia miungu yao; kwa maana hata wana wao na binti zao huiteketezea hiyo miungu yao ndani ya moto.


Basi nikamtwaa huyo suria wangu, na kumkata vipande, na kumpeleka katika nchi yote ya urithi wa Israeli; kwa sababu wametenda maovu makuu na upumbavu katika Israeli.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo