Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Walawi 16:30 - Swahili Revised Union Version

30 Kwa maana siku hiyo upatanisho utafanywa kwa ajili yenu, ili kuwatakasa; nanyi mtatakaswa na dhambi zenu zote mbele za BWANA.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

30 Mtafanya hivyo kwa sababu siku hiyo ndiyo siku ambayo mtafanyiwa ibada ya upatanisho, msafishwe dhambi zenu, nanyi mtakuwa safi mbele ya Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

30 Mtafanya hivyo kwa sababu siku hiyo ndiyo siku ambayo mtafanyiwa ibada ya upatanisho, msafishwe dhambi zenu, nanyi mtakuwa safi mbele ya Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

30 Mtafanya hivyo kwa sababu siku hiyo ndiyo siku ambayo mtafanyiwa ibada ya upatanisho, msafishwe dhambi zenu, nanyi mtakuwa safi mbele ya Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

30 kwa sababu siku hii upatanisho utafanyika kwa ajili yenu ili kuwatakasa. Kisha mtakuwa safi mbele za Mwenyezi Mungu kutokana na dhambi zenu zote.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

30 kwa sababu siku hii upatanisho utafanyika kwa ajili yenu ili kuwatakasa. Kisha mtakuwa safi mbele za bwana kutokana na dhambi zenu zote.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

30 Kwa maana siku hiyo upatanisho utafanywa kwa ajili yenu, ili kuwatakasa; nanyi mtatakaswa na dhambi zenu zote mbele za BWANA.

Tazama sura Nakili

Walawi 16:30
12 Marejeleo ya Msalaba  

Ee Mungu, uniumbie moyo safi, Uifanye upya na kuithibiti roho yangu.

Unioshe kabisa uovu wangu, Unitakase dhambi zangu.

Unisafishe kwa hisopo nami nitakuwa safi, Unioshe, nami nitakuwa mweupe kuliko theluji.

Nami nitawasafisha uovu wao wote, ambao kwao wamenitenda dhambi; nami nitawasamehe maovu yao yote, ambayo kwayo wamenitenda dhambi, na kukosa juu yangu.

Lakini siku ya kumi ya mwezi huo wa saba ni siku ya upatanisho; itakuwa kusanyiko takatifu kwenu, nanyi mtajinyima; na mtatoa sadaka kwa BWANA kwa njia ya moto.

Na msifanye kazi yoyote siku hiyo; kwa kuwa ni siku ya upatanisho, ili kufanya upatanisho kwa ajili yenu mbele za BWANA, Mungu wenu.

ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno;

ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili yetu, ili atukomboe na maasi yote, na kujisafishia watu wake mwenyewe walio na bidii katika matendo mema.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo