Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Walawi 16:3 - Swahili Revised Union Version

3 Haruni ataingia katika patakatifu na vitu hivi; ng'ombe dume mchanga kwa sadaka ya dhambi, na kondoo dume kwa sadaka ya kuteketezwa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 Aroni ataingia mahali patakatifu sana akiwa na fahali mchanga kwa ajili ya sadaka ya kuondoa dhambi na kondoo dume kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

3 Aroni ataingia mahali patakatifu sana akiwa na fahali mchanga kwa ajili ya sadaka ya kuondoa dhambi na kondoo dume kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 Aroni ataingia mahali patakatifu sana akiwa na fahali mchanga kwa ajili ya sadaka ya kuondoa dhambi na kondoo dume kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 “Hivi ndivyo Haruni atakavyoingia katika Mahali Patakatifu: atachukua fahali mchanga kwa ajili ya sadaka ya dhambi, na kondoo dume kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

3 “Hivi ndivyo Haruni atakavyoingia katika mahali patakatifu: atachukua fahali mchanga kwa ajili ya sadaka ya dhambi, na kondoo dume kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

3 Haruni ataingia katika patakatifu na vitu hivi; ng'ombe dume mchanga kwa sadaka ya dhambi, na kondoo dume kwa sadaka ya kuteketezwa.

Tazama sura Nakili




Walawi 16:3
13 Marejeleo ya Msalaba  

Na matoleo yake kwamba ni katika kundi, katika kondoo, au katika mbuzi, kuwa sadaka ya kuteketezwa; atatoa dume asiye na dosari.


Ikawa matoleo yake ni sadaka ya kuteketezwa ya ng'ombe, atatoa ng'ombe dume mkamilifu; ataleta mlangoni pa hema ya kukutania, ili akubaliwe mbele ya BWANA.


Na Haruni atamtoa yule ng'ombe wa sadaka ya dhambi, aliye kwa ajili ya nafsi yake, na kufanya upatanisho kwa ajili ya nafsi yake mwenyewe, na kwa ajili ya nyumba yake.


BWANA akanena na Musa, na kumwambia,


kama kuhani aliyetiwa mafuta akifanya dhambi, hata analeta hatia juu ya watu; ndipo na atoe kwa ajili ya dhambi yake aliyoifanya, na kumsongeza kwa BWANA ng'ombe dume mchanga mkamilifu, kuwa ni sadaka ya dhambi.


Kisha akamleta yule ng'ombe dume wa sadaka ya dhambi; na Haruni na wanawe wakaweka mikono yao katika kichwa cha huyo ng'ombe wa sadaka ya dhambi.


Kisha akamsongeza yule kondoo dume wa sadaka ya kuteketezwa; na Haruni na wanawe wakaweka mikono yao kichwani mwa huyo kondoo.


akamwambia Haruni, Twaa wewe mwana-ng'ombe wa kiume awe sadaka ya dhambi, na kondoo dume wa sadaka ya kuteketezwa, wakamilifu, ukawasongeze mbele ya BWANA.


Nawe utawaambia wana wa Israeli, ukisema, Twaeni mbuzi dume awe sadaka ya dhambi; na mwana-ng'ombe, na mwana-kondoo, wote wa mwaka wa kwanza, wakamilifu, kwa sadaka ya kuteketezwa;


wala si kwa damu ya mbuzi na ndama, bali kwa damu yake mwenyewe aliingia mara moja tu katika Patakatifu, akiisha kupata ukombozi wa milele.


Lakini katika hema hiyo ya pili kuhani mkuu huingia peke yake, mara moja kila mwaka; wala si pasipo damu, atoayo kwa ajili ya nafsi yake na kwa dhambi walizozitenda hao watu bila kujua.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo