Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Walawi 16:24 - Swahili Revised Union Version

24 naye ataosha mwili wake kwa maji mahali patakatifu, na kuvaa nguo zake, na kutoka, na kusongeza sadaka ya kuteketezwa yake mwenyewe, na sadaka ya kuteketezwa ya watu, naye atafanya upatanisho kwa ajili ya nafsi yake, na kwa ajili ya watu.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

24 Ataoga humo ndani katika mahali patakatifu na kuvaa mavazi yake. Atatoka na kutoa sadaka yake ya kuteketezwa, na sadaka ya kuteketezwa ya watu wa Israeli, ili kufanya ibada ya upatanisho kwa ajili yake mwenyewe na kwa ajili ya watu wote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

24 Ataoga humo ndani katika mahali patakatifu na kuvaa mavazi yake. Atatoka na kutoa sadaka yake ya kuteketezwa, na sadaka ya kuteketezwa ya watu wa Israeli, ili kufanya ibada ya upatanisho kwa ajili yake mwenyewe na kwa ajili ya watu wote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

24 Ataoga humo ndani katika mahali patakatifu na kuvaa mavazi yake. Atatoka na kutoa sadaka yake ya kuteketezwa, na sadaka ya kuteketezwa ya watu wa Israeli, ili kufanya ibada ya upatanisho kwa ajili yake mwenyewe na kwa ajili ya watu wote.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

24 Ataoga kwa maji katika mahali patakatifu na kuvaa mavazi yake ya kawaida. Kisha atatoka na kutoa dhabihu ya sadaka ya kuteketezwa kwa ajili yake na sadaka ya kuteketezwa kwa ajili ya watu, ili kufanya upatanisho kwa ajili yake mwenyewe, na kwa ajili ya watu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

Walawi 16:24
14 Marejeleo ya Msalaba  

Kisha utafanya kanzu kwa ajili ya wana wa Haruni, nawe wafanyie mishipi, wafanyie na kofia kwa utukufu na uzuri.

Nawe mvike huyo nduguyo Haruni na wanawe nao mavazi hayo; nawe watie mafuta, na kuwaweka kwa kazi takatifu, na kuwatakasa, ili wapate kunitumikia mimi katika kazi ya ukuhani.

Makuhani watakapoingia ndani, hawatatoka mahali patakatifu kwenda hadi katika ua wa nje; lakini wataweka mavazi yao katika mahali wahudumiapo; maana ni matakatifu; nao watavaa mavazi mengine, na kupakaribia mahali pa wazi kwa watu.

Kisha siku ya saba atanyoa nywele zote za kichwani mwake, na ndevu zake, na nyusi zake, nywele zake zote pia atazinyoa; kisha atazifua nguo zake, na kuoga mwili wake majini, naye atakuwa safi.

Na mafuta ya sadaka ya dhambi atayateketeza juu ya madhabahu.

huyo mtu atakayegusa kitu chochote namna hiyo atakuwa najisi hata jioni, naye hatakula katika vitu vitakatifu, asipooga mwili wake majini.

Musa akamwambia Haruni, Ikaribie madhabahu, uitoe sadaka yako ya dhambi, na sadaka yako ya kuteketezwa, ukafanye upatanisho kwa ajili ya nafsi yako, na kwa ajili ya watu; nawe uitoe hiyo dhabihu ya watu, ukafanye upatanisho kwa ajili yao; kama BWANA alivyoagiza.

kwa kuwa ni sheria za jinsi ya mwili tu, vyakula na vinywaji na kunawa kwingine kwingine, zilizoamriwa hata wakati wa matengenezo mapya.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo