Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Walawi 14:8 - Swahili Revised Union Version

8 Naye huyo atakayetakaswa atazifua nguo zake, na kunyoa nywele zake zote, na kuoga katika maji, naye atakuwa safi; baada ya hayo ataingia ndani ya kambi, lakini ataketi nje ya hema yake muda wa siku saba.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

8 Huyo mtu atayafua mavazi yake, atanyoa nywele zake, na kuoga; naye atakuwa safi. Baada ya hayo atarudi kambini, lakini atakaa nje ya hema lake kwa muda wa siku saba.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

8 Huyo mtu atayafua mavazi yake, atanyoa nywele zake, na kuoga; naye atakuwa safi. Baada ya hayo atarudi kambini, lakini atakaa nje ya hema lake kwa muda wa siku saba.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

8 Huyo mtu atayafua mavazi yake, atanyoa nywele zake, na kuoga; naye atakuwa safi. Baada ya hayo atarudi kambini, lakini atakaa nje ya hema lake kwa muda wa siku saba.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

8 “Huyo mtu atakayetakaswa ni lazima afue nguo zake, anyoe nywele zake zote, na aoge kwa maji; ndipo atakapotakasika. Baada ya hili anaweza kuingia kambini, lakini ni lazima akae nje ya hema lake kwa siku saba.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

8 “Huyo mtu atakayetakaswa ni lazima afue nguo zake, anyoe nywele zake zote, na aoge kwa maji; ndipo atakapokuwa safi kwa desturi ya ibada. Baada ya hili anaweza kuingia kambini, lakini ni lazima akae nje ya hema lake kwa siku saba.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

8 Naye huyo atakayetakaswa atazifua nguo zake, na kunyoa nywele zake zote, na kuoga katika maji, naye atakuwa safi; baada ya hayo ataingia ndani ya kambi, lakini ataketi nje ya hema yake muda wa siku saba.

Tazama sura Nakili




Walawi 14:8
19 Marejeleo ya Msalaba  

Uzia mfalme akawa na ukoma hadi siku ya kufa kwake, akakaa katika nyumba ya pekee, kwa kuwa ni mwenye ukoma; maana alitengwa na nyumba ya BWANA; na Yothamu mwanawe alikuwa kiongozi wa nyumba ya mfalme, akiwatawala watu wa nchi.


BWANA akamwambia Musa, Nenda kwa watu hawa, ukawatakase leo na kesho, wakazifue nguo zao,


Musa akateremka mlimani akawaendea watu akawatakasa, nao wakafua nguo zao.


na mtu awaye yote atakayechukua chochote cha mizoga yao atafua nguo zake, naye atakuwa najisi hata jioni.


kisha kuhani ataisongeza hiyo sadaka ya kuteketezwa, na sadaka ya unga, juu ya madhabahu na kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake, naye atakuwa safi.


Kisha siku ya saba atanyoa nywele zote za kichwani mwake, na ndevu zake, na nyusi zake, nywele zake zote pia atazinyoa; kisha atazifua nguo zake, na kuoga mwili wake majini, naye atakuwa safi.


Na huyo aliye na kisonono atakapotakaswa na kisonono chake, atajihesabia siku saba kwa kutakaswa kwake, naye atazifua nguo zake; naye ataoga mwili wake katika maji ya mtoni, naye atakuwa safi.


Basi Musa akawaleta Haruni na wanawe, akawaosha kwa maji.


Na kama mtu yeyote akifa ghafla karibu naye, akajitia unajisi kichwa cha kutengwa kwake, ndipo atakinyoa kichwa siku hiyo ya kutakaswa kwake, atakinyoa siku ya saba.


Nawe utawafanyia mambo haya ili kuwatakasa; nyunyiza juu yao maji yatakasayo dhambi, nao wajinyoe kwa wembe mwili wote, kisha wazifue nguo zao, na kujitakasa.


ndipo umchukue kwenu nyumbani kwako, naye atanyoa kichwa, akate na kucha;


Mfano wa mambo hayo ni ubatizo, unaowaokoa ninyi pia siku hizi; (siyo kuwekea mbali uchafu wa mwili, bali jibu la dhamiri safi mbele za Mungu), kwa kufufuka kwake Yesu Kristo.


Nikamwambia, Bwana wangu, wajua wewe. Akaniambia, Hao ndio wanatoka katika dhiki ile iliyo kuu, nao wamefua mavazi yao, na kuyafanya meupe katika damu ya Mwana-kondoo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo