Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Walawi 14:25 - Swahili Revised Union Version

25 kisha atamchinja mwana-kondoo wa sadaka ya hatia, na kuhani atatwaa katika damu ya sadaka ya hatia, na kuitia katika ncha ya sikio la kulia la huyo atakayetakaswa, na katika kidole cha gumba cha mkono wake wa kulia, na katika kidole kikuu cha mguu wake wa kulia;

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

25 Atamchinja huyo mwanakondoo dume wa sadaka ya kuondoa hatia. Kuhani atachukua kiasi cha damu na kumpaka huyo mtu anayetakaswa katika ncha ya sikio lake la kulia, katika kidole gumba cha mkono wake wa kulia na kidole gumba cha mguu wake wa kulia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

25 Atamchinja huyo mwanakondoo dume wa sadaka ya kuondoa hatia. Kuhani atachukua kiasi cha damu na kumpaka huyo mtu anayetakaswa katika ncha ya sikio lake la kulia, katika kidole gumba cha mkono wake wa kulia na kidole gumba cha mguu wake wa kulia.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

25 Atamchinja huyo mwana-kondoo kwa ajili ya sadaka ya hatia. Kisha ataichukua sehemu ya damu yake na kuipaka kwenye ncha ya sikio la kuume la yule anayetakaswa, na aipake pia kwenye kidole gumba cha mkono wa kuume wa huyo mtu, na kidole kikubwa cha mguu wake wa kuume.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

25 Atamchinja huyo mwana-kondoo kwa ajili ya sadaka ya hatia. Pia ataichukua sehemu ya damu yake na kuipaka kwenye ncha ya sikio la kuume la yule anayetakaswa, na aipake pia kwenye kidole gumba cha mkono wa kuume wa huyo mtu, na kidole kikubwa cha mguu wake wa kuume.

Tazama sura Nakili

Walawi 14:25
7 Marejeleo ya Msalaba  

Dhabihu na matoleo hukupendezwa nazo, Umetuzidishia ila masikio, Kafara na sadaka za dhambi hukuzitaka.

Kisha utamchinja kondoo, na kuitwaa damu yake, na kuitia katika ncha ya sikio la Haruni la upande wa kulia, na katika ncha za masikio ya kulia ya wanawe, na katika vyanda vya gumba vya mikono yao ya kulia, na katika vidole vikuu vya miguu yao ya kulia, na kuinyunyiza hiyo damu katika madhabahu kuizunguka kandokando.

Jitunze mguu wako uendapo nyumbani kwa Mungu; Maana ni heri kukaribia ili usikie, Kuliko kutoa kafara ya wapumbavu; Ambao hawajui kuwa wafanya mabaya.

kisha kuhani atajimiminia baadhi ya mafuta hayo katika kitanga cha mkono wake wa kushoto;

Lakini asipomweza mwana-kondoo, ndipo atakapomletea BWANA hua wawili, au makinda mawili ya njiwa, kuwa ni sadaka yake ya hatia ya jambo hilo alilolikosa; mmoja wa hao ndege kwa sadaka ya dhambi, na wa pili kwa sadaka ya kuteketezwa.

Kisha akamchinja; na Musa akatwaa baadhi ya damu yake, na kuitia katika ncha ya sikio la kulia la Haruni, na katika kidole cha gumba cha mkono wake wa kulia, na katika kidole cha gumba cha guu lake la kulia.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo