Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Walawi 11:31 - Swahili Revised Union Version

31 Wanyama hao ndio walio najisi kwenu katika hao watambaao; yeyote atakayewagusa, wakiisha kuwa mgoza, atakuwa ni najisi hata jioni.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

31 Hao wote ni najisi kwenu na yeyote atakayegusa mizoga yao, atakuwa najisi mpaka jioni.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

31 Hao wote ni najisi kwenu na yeyote atakayegusa mizoga yao, atakuwa najisi mpaka jioni.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

31 Hao wote ni najisi kwenu na yeyote atakayegusa mizoga yao, atakuwa najisi mpaka jioni.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

31 Miongoni mwa wanyama wote wanaotambaa juu ya ardhi, hawa ni najisi kwenu. Yeyote agusaye mizoga yao atakuwa najisi hadi jioni.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

31 Hao wote watambaao juu ya ardhi ni najisi kwenu. Yeyote agusaye mizoga yao atakuwa najisi mpaka jioni.

Tazama sura Nakili




Walawi 11:31
11 Marejeleo ya Msalaba  

Mungu akasema, Maji na yajawe kwa wingi na viumbe vyenye uhai, na ndege waruke juu ya nchi katika anga la mbingu.


na guruguru kenge, mjusi, goromoe na lumbwi.


Tena kitu chochote, wanyama hao mmojawapo atakachokiangukia, wakiisha kufa, kitakuwa ni najisi; cha mti, nguo, ngozi, gunia, chombo chochote cha kufanyia kazi yoyote, lazima kitiwe ndani ya maji, nacho kitakuwa ni najisi hadi jioni; ndipo kitakapokuwa ni safi.


Msiile nyama yao, wala msiiguse mizoga yao; hao ni najisi kwenu.


Tena mtu atakayeingia ndani ya hiyo nyumba wakati huo wote iliofungwa, atakuwa najisi hadi jioni.


na kuhani atawasongeza, mmoja kuwa sadaka ya dhambi, na wa pili kuwa sadaka ya kuteketezwa; naye kuhani atafanya upatanisho mbele za BWANA kwa ajili ya kisonono chake.


Na mtu yule amwachaye mbuzi wa Azazeli aende zake, ataosha nguo zake, na kuosha mwili wake kwa maji, na baadaye ataingia katika kambi.


Tena kila mtu atakayekula nyamafu, au nyama ya mnyama aliyeraruliwa na wanyama, awe ni mzalia au mgeni, atafua nguo zake, na kuoga majini naye atakuwa najisi hadi jioni; ndipo atakapokuwa safi.


huyo mtu atakayegusa kitu chochote namna hiyo atakuwa najisi hata jioni, naye hatakula katika vitu vitakatifu, asipooga mwili wake majini.


Ndipo kuhani atazifua nguo zake, na kuoga mwili wake majini, kisha baadaye ataingia kambini, naye kuhani atakuwa najisi hadi jioni.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo