Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Waebrania 9:1 - Swahili Revised Union Version

1 Basi hata agano la kwanza lilikuwa na kawaida za ibada, na patakatifu pake, pa kidunia.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Agano la kwanza lilikuwa na taratibu zake za ibada na maskani takatifu ya duniani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Agano la kwanza lilikuwa na taratibu zake za ibada na maskani takatifu ya duniani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Agano la kwanza lilikuwa na taratibu zake za ibada na maskani takatifu ya duniani.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Basi agano lile la kwanza lilikuwa na kanuni zake za kuabudu na pia patakatifu pake pa kidunia.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Basi agano lile la kwanza lilikuwa na kanuni zake za kuabudu na pia patakatifu pake pa kidunia.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

1 Basi hata agano la kwanza lilikuwa na kawaida za ibada, na patakatifu pake, pa kidunia.

Tazama sura Nakili




Waebrania 9:1
14 Marejeleo ya Msalaba  

Nao na wanifanyie patakatifu; ili nipate kukaa kati yao.


Na ikiwa wameyatahayarikia yote waliyoyatenda, waoneshe umbo la nyumba, na namna yake, na matokeo yake, na maingilio yake, na maumbo yake yote, na maagizo yake yote, na kawaida zake zote, na sheria zake zote, ukayaandike machoni pao; ili walishike umbo lake lote, na maagizo yake, na kuyatenda.


Kwa hiyo yafuateni maagizo yangu, ili kamwe msiwe na mojawapo ya tabia hizi zinazochukiza, zilizotangulia kufanywa mbele zenu; mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.


Basi kwa hiyo watayashika maagizo yangu, wasije wakachukua dhambi kwa hayo, nao wakafa humo, wakiyanajisi; mimi ndimi BWANA niwatakasaye.


wasisaze kitu chake chochote hadi asubuhi, wala wasimvunje mfupa wake; kama hiyo sheria yote ya Pasaka ilivyo ndivyo watakavyoishika.


Na wote wawili walikuwa wenye haki mbele za Mungu, wakiishi katika amri zote za Bwana na maagizo yake bila lawama.


ambao ni Waisraeli, wenye kule kufanywa wana, na ule utukufu, na maagano, na kupewa torati, na ibada ya Mungu, na ahadi zake;


Angalieni mtu asiwafanye mateka kwa elimu yake ya bure na madanganyo matupu, kwa jinsi ya mapokeo ya wanadamu, kwa jinsi ya mafundisho ya awali ya ulimwengu, wala si kwa jinsi ya Kristo.


Kwa kule kusema, Agano jipya, amelifanya lile la kwanza kuwa kuukuu. Lakini kitu kianzacho kuwa kikuukuu na kuchakaa kiko karibu kutoweka.


mhudumu wa patakatifu, na wa ile hema ya kweli, ambayo Bwana aliiweka wala si mwanadamu.


Maana kama lile la kwanza lingalikuwa halina upungufu, nafasi isingalitafutwa kwa lile la pili.


Kwa sababu Kristo hakuingia katika patakatifu palipofanyika kwa mikono, ndio mfano wa patakatifu halisi; bali aliingia mbinguni hasa, aonekane sasa usoni pa Mungu kwa ajili yetu;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo