Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Waebrania 7:1 - Swahili Revised Union Version

1 Kwa maana Melkizedeki huyo, mfalme wa Salemu, kuhani wa Mungu aliye juu, aliyekutana na Abrahamu alipokuwa akirudi katika kuwapiga hao wafalme, akambariki;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Huyo Melkisedeki alikuwa mfalme wa Salemu, na kuhani wa Mungu Mkuu. Abrahamu alipokuwa anarudi kutoka vitani ambako aliwaua wafalme, Melkisedeki alikutana naye, akambariki,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Huyo Melkisedeki alikuwa mfalme wa Salemu, na kuhani wa Mungu Mkuu. Abrahamu alipokuwa anarudi kutoka vitani ambako aliwaua wafalme, Melkisedeki alikutana naye, akambariki,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Huyo Melkisedeki alikuwa mfalme wa Salemu, na kuhani wa Mungu Mkuu. Abrahamu alipokuwa anarudi kutoka vitani ambako aliwaua wafalme, Melkisedeki alikutana naye, akambariki,

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Kwa kuwa huyu Melkizedeki alikuwa mfalme wa Salemu na kuhani wa Mungu Aliye Juu Sana. Alipokutana na Ibrahimu akirudi kutoka kuwashinda wafalme, Melkizedeki alimbariki,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Kwa kuwa huyu Melkizedeki alikuwa mfalme wa Salemu na kuhani wa Mungu Aliye Juu Sana. Alipokutana na Ibrahimu akirudi kutoka kuwashinda hao wafalme, Melkizedeki alimbariki,

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

1 Kwa maana Melkizedeki huyo, mfalme wa Salemu, kuhani wa Mungu aliye juu, aliyekutana na Abrahamu alipokuwa akirudi katika kuwapiga hao wafalme, akambariki;

Tazama sura Nakili




Waebrania 7:1
17 Marejeleo ya Msalaba  

Nitamwita MUNGU Aliye Juu, Mungu anitimiziaye mambo yangu.


Kibanda chake pia kiko Salemu, Na maskani yake iko Sayuni.


Wakakumbuka kuwa Mungu ni mwamba wao, Na Mungu Aliye Juu ni mkombozi wao.


Lakini walimjaribu Mungu Aliye Juu, wakamwasi, Wala hawakuzishika shuhuda zake.


Mimi nimeona vema kutangaza habari za ishara na maajabu, aliyonitendea Mungu aliye juu.


Kwa habari zako, Ee mfalme, Mungu Aliye Juu alimpa Nebukadneza, baba yako, ufalme, na ukuu, na fahari, na utukufu;


Akafukuzwa mbali na wanadamu, moyo wake ukafanywa kuwa kama moyo wa mnyama, na makao yake yalikuwa pamoja na punda mwitu; akalishwa majani kama ng'ombe, mwili wake ukalowa maji kwa umande wa mbinguni; hata alipojua ya kuwa Mungu Aliye Juu ndiye anayetawala katika ufalme wa wanadamu, na ya kuwa humweka juu yake yeye amtakaye, awaye yote.


Nimwendee BWANA na kitu gani, na kuinama mbele za Mungu aliye juu? Je! Nimwendee na sadaka za kuteketezwa, na ndama wa umri wa mwaka mmoja?


akapiga kelele kwa sauti kuu, akasema, Nina nini nawe, Yesu, Mwana wa Mungu aliye juu? Nakuapisha kwa Mungu usinitese.


Akamfuata Paulo na sisi akipiga kelele, akisema, Watu hawa ni watumishi wa Mungu aliye juu, wenye kuwahubiria njia ya wokovu.


alimoingia Yesu kwa ajili yetu, mtangulizi wetu, amekuwa kuhani mkuu hata milele kwa mfano wa Melkizedeki.


ambaye Abrahamu alimgawia sehemu ya kumi ya vitu vyote; (tafsiri ya jina lake kwanza ni mfalme wa haki, tena, mfalme wa Salemu, maana yake, mfalme wa amani;


hana baba, hana mama, hana wazazi, hana mwanzo wa siku zake, wala mwisho wa uhai wake, bali amefananishwa na Mwana wa Mungu); huyo adumu kuhani milele.


Bali yeye, ambaye uzazi wake haukuhesabiwa kuwa umetoka kwa hao, alitwaa sehemu ya kumi kwa Abrahamu, akambariki yeye aliye na ile ahadi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo