Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Waebrania 6:7 - Swahili Revised Union Version

7 Maana nchi inayoinywa mvua inayoinyeshea mara kwa mara, na kuzaa mboga zenye manufaa kwa hao ambao kwa ajili yao inalimwa, hupokea baraka zitokazo kwa Mungu;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

7 Ardhi ambayo huipokea mvua inayoinyeshea mara kwa mara na kuotesha mimea ya faida kwa mkulima imebarikiwa na Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

7 Ardhi ambayo huipokea mvua inayoinyeshea mara kwa mara na kuotesha mimea ya faida kwa mkulima imebarikiwa na Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

7 Ardhi ambayo huipokea mvua inayoinyeshea mara kwa mara na kuotesha mimea ya faida kwa mkulima imebarikiwa na Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

7 Ardhi inayopokea mvua inayonyesha mara kwa mara juu yake na baadaye inatoa mazao ya kuwanufaisha wale ambao inalimwa kwa ajili yao, hupokea baraka za Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

7 Ardhi ile ipokeayo mvua inyeshayo juu yake mara kwa mara hutoa mazao yanayowanufaisha wale ambao kwa ajili yao yalimwa, nayo nchi hiyo hupokea baraka kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

7 Maana nchi inayoinywa mvua inayoinyeshea mara kwa mara, na kuzaa mboga zenye manufaa kwa hao ambao kwa ajili yao inalimwa, hupokea baraka zitokazo kwa Mungu;

Tazama sura Nakili




Waebrania 6:7
17 Marejeleo ya Msalaba  

Mungu akasema, Nchi na itoe majani, mimea itoayo mbegu, na miti ya matunda izaayo matunda kwa jinsi yake, ambao mbegu zake zimo ndani yake, juu ya nchi; ikawa hivyo.


Akakaribia akambusu. Naye akasikia harufu ya mavazi yake, akambariki akasema, Tazama, harufu ya mwanangu Ni kama harufu ya shamba alilolibariki Bwana.


Ingawa mtu anakwenda zake akilia, Azichukuapo mbegu za kupanda. Hakika atarudi kwa kelele za furaha, Aichukuapo miganda yake.


Atapokea baraka kwa BWANA, Na haki kwa Mungu wa wokovu wake.


Kwa maana nitamimina maji juu yake aliye na kiu, na vijito vya maji juu ya mahali pakavu; nitamwaga roho yangu juu ya wazao wako, na baraka yangu juu yao utakaowazaa;


Nami nitawafanya wao, na mahali palipo pande zote za mlima wangu, kuwa baraka, nami nitaleta manyunyu kwa wakati wake; yatakuwako manyunyu ya baraka.


Jipandieni katika haki, vuneni kwa fadhili; uchimbueni udongo wa mashamba yenu, kwa maana wakati umewadia wa kumtafuta BWANA, hata atakapokuja na kuwanyeshea haki.


ndipo nitawaamria baraka yangu iwe juu yenu mwaka wa sita, nayo inchi itazaa matunda ya kutosha miaka mitatu.


Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema BWANA wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.


kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa.


Yampasa mkulima mwenye bidii ya kazi kuwa wa kwanza wa kupata fungu la mavuno.


Kwa hiyo ndugu, vumilieni, hata kuja kwake Bwana. Tazama, mkulima hungoja mazao ya nchi yaliyo ya thamani, huvumilia kwa ajili yake hata yatakapopata mvua ya kwanza na ya mwisho.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo