Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Waamuzi 6:1 - Swahili Revised Union Version

1 Kisha wana wa Israeli walifanya yaliyo maovu mbele za macho ya BWANA; BWANA akawatia mikononi mwa Midiani muda wa miaka saba

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Waisraeli walitenda uovu mbele ya Mwenyezi-Mungu; naye akawatia mikononi mwa Wamidiani kwa muda wa miaka saba.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Waisraeli walitenda uovu mbele ya Mwenyezi-Mungu; naye akawatia mikononi mwa Wamidiani kwa muda wa miaka saba.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Waisraeli walitenda uovu mbele ya Mwenyezi-Mungu; naye akawatia mikononi mwa Wamidiani kwa muda wa miaka saba.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Waisraeli wakafanya tena yaliyo maovu mbele za Mwenyezi Mungu, naye Mwenyezi Mungu akawatia mikononi mwa Wamidiani kwa muda wa miaka saba.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Waisraeli wakafanya tena yaliyo maovu mbele za bwana, naye kwa miaka saba bwana akawatia mikononi mwa Wamidiani.

Tazama sura Nakili




Waamuzi 6:1
16 Marejeleo ya Msalaba  

Akamzalia Zimrani, na Yokshani, na Medani, na Midiani, na Ishbaki, na Sua.


Wakapita wafanya biashara Wamidiani; basi wakamtoa Yusufu, wakampandisha kumtoa katika shimo, wakamuuza Yusufu kwa Waishmaeli kwa vipande vya fedha ishirini; nao wakamchukua Yusufu mpaka Misri.


Niliziona hema za Kushani zikitaabika; Mapazia ya nchi ya Midiani yakatetemeka.


Moabu akawaambia wazee wa Midiani, Sasa jeshi hili la watu litaramba vitu vyote vinavyotuzunguka, kama vile ng'ombe arambavyo majani ya mashamba. Na Balaki, mwana wa Sipori, alikuwa mfalme wa Moabu zamani zile.


Nami niseme nini tena? Maana wakati usingenitosha kuleta habari za Gideoni na Baraka na Samsoni na Yeftha na Daudi na Samweli na za manabii;


Hasira za BWANA ziliwaka juu ya Israeli, akawauza na kuwaua mikononi mwa Wafilisti, na mikononi mwa wana wa Amoni.


Wana wa Israeli walifanya mambo maovu mbele za macho ya BWANA, na wakawatumikia Mabaali.


Gideoni akamwambia, Ee Bwana wangu, ikiwa BWANA yu pamoja nasi, mbona mambo haya yote yametupata? Yako wapi matendo yake ya ajabu, waliyotuhadithia baba zetu, wakisema, Je! Siye BWANA, aliyetuleta huku kutoka Misri? Ila sasa ametutupa, naye ametutia katika mikono ya Midiani.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo