Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Waamuzi 18:4 - Swahili Revised Union Version

4 Naye akawaambia, Hivi na hivi ndivyo alivyonifanyia Mika, ameniajiri, nami nimekuwa kuhani wake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 Yeye akawajibu, “Mika amefanya nami mpango; ameniajiri nami nimekuwa kuhani wake.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 Yeye akawajibu, “Mika amefanya nami mpango; ameniajiri nami nimekuwa kuhani wake.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 Yeye akawajibu, “Mika amefanya nami mpango; ameniajiri nami nimekuwa kuhani wake.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 Akawaeleza yale Mika aliyomtendea, akasema, “Ameniajiri, nami ni kuhani wake.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 Akawaeleza yale Mika aliyomtendea, naye akasema, “Ameniajiri nami ni kuhani wake.”

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

4 Naye akawaambia, Hivi na hivi, ndivyo alivyonifanyia Mika, ameniajiri, nami nimekuwa kuhani wake.

Tazama sura Nakili




Waamuzi 18:4
16 Marejeleo ya Msalaba  

Kupendelea watu si kwema; Wala mtu kuasi kwa ajili ya kipande cha mkate.


Naam, mbwa hao wana uchu sana, hawashibi kamwe; na hao ni wachungaji wasioweza kufahamu neno; wote pia wamegeuka upande, wazifuate njia zao wenyewe, kila mmoja kwa faida yake, toka pande zote.


Nanyi mmeninajisi kati ya watu wangu, kwa ajili ya makonzi ya shayiri na vipande vya mkate, ili kuziua roho za watu ambao haiwapasi kufa, na kuzihifadhi hai roho za watu ambao haikuwapasa kuwa hai, kwa kuwaambia uongo watu wangu wasikilizao uongo.


Laiti angekuwapo kwenu mtu mmoja wa kuifunga milango; msije mkawasha moto bure madhabahuni pangu! Sina furaha kwenu, asema BWANA wa majeshi, wala sitakubali dhabihu yoyote mikononi mwenu.


Sikutamani fedha wala dhahabu, wala mavazi ya mtu.


asiwe mtu wa kulewa, asiye dhalimu; bali awe mpole; asiwe mbishi, wala asiwe mwenye kupenda fedha;


Hao wanapindua watu wa nyumba nzima, wakifundisha yasiyowapasa kwa ajili ya mapato ya aibu.


Na kwa tamaa yao watajipatia faida kwenu kwa maneno yaliyotungwa; wao ambao hukumu yao tangu zamani haikawii, wala maangamizi yao hayasinzii.


Mika akamwambia, kaa pamoja nami, uwe kwangu baba, tena kuhani, nami nitakupa fedha kumi kila mwaka, na nguo ya kuvaa, na vyakula. Basi huyo Mlawi akaingia ndani.


Basi Mika akamweka wakfu huyo Mlawi, huyo kijana, naye akawa kuhani wake, akakaa nyumbani mwa Mika.


Basi hapo walipokuwa karibu na nyumba ya Mika, wakatambua sauti yake huyo kijana Mlawi; ndipo wakageuka wakaenda kuko, na kumwuliza, Je! Ni nani aliyekuleta wewe huku? Unafanya nini mahali hapa? Una kazi gani hapa?


Nao wakamwambia, Tafadhali tutakie shauri la Mungu, ili tupate kujua kama njia yetu tuiendeayo itafanikiwa.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo