Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Waamuzi 1:9 - Swahili Revised Union Version

9 Baadaye wana wa Yuda wakateremka ili wapigane na hao Wakanaani waliokaa katika nchi yenye milima, na nchi ya Negebu, na nchi ya Shefela.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 Baadaye, watu wa kabila la Yuda walikwenda kupigana na Wakanaani walioishi kwenye nchi ya milima, Negebu na kwenye nchi tambarare.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

9 Baadaye, watu wa kabila la Yuda walikwenda kupigana na Wakanaani walioishi kwenye nchi ya milima, Negebu na kwenye nchi tambarare.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 Baadaye, watu wa kabila la Yuda walikwenda kupigana na Wakanaani walioishi kwenye nchi ya milima, Negebu na kwenye nchi tambarare.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 Baada ya hayo, watu wa Yuda wakateremka kupigana na Wakanaani walioishi katika nchi ya vilima, na Negebu, na nchi ya Shefela.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

9 Baada ya hayo, watu wa Yuda wakateremka kupigana na Wakanaani walioishi katika nchi ya vilima, yaani, Negebu na nchi chini ya vilima vya magharibi.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

9 Baadaye wana wa Yuda wakateremka ili wapigane na hao Wakanaani waliokaa katika nchi yenye milima, na nchi ya Negebu, na nchi ya Shefela.

Tazama sura Nakili

Waamuzi 1:9
7 Marejeleo ya Msalaba  

Naye Abramu akasafiri, akazidi kwenda pande za kusini.

Kisha Yoshua akakwea kutoka hapo Egloni, na Israeli wote pamoja naye, hadi wakafika Hebroni; nao wakapigana nao;

Wakati huo Yoshua akaenda na kuwakatilia mbali hao Waanaki watoke nchi ya vilima, kutoka Hebroni, na kutoka Debiri, na kutoka Anabu, na kutoka katika nchi yote ya vilima vilima ya Yuda, na kutoka katika nchi yote ya vilima vilima ya Israeli; Yoshua akawaangamiza kabisa na miji yao.

katika nchi ya vilima, na katika Shefela, na katika nchi ya Araba, na katika materemko, na katika nyika, na katika Negebu; nchi ya Mhiti, na Mwamori, na Mkanaani, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi;

Kisha Yuda akawafuatia hao Wakanaani waliokaa katika Hebroni; (jina la Hebroni hapo kwanza ulikuwa ukiitwa Kiriath-arba;) nao wakamwua Sheshai, na Ahimani, na Talmai.

Kisha wana wa Yuda wakapigana na Yerusalemu, wakautwaa, wakaupiga kwa makali ya upanga, na kuupiga moto huo mji.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo