Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Ufunuo 7:3 - Swahili Revised Union Version

3 akisema, Msiidhuru nchi, wala bahari, wala miti, hadi tutakapokwisha kuwatia mhuri watumishi wa Mungu wetu juu ya vipaji vya nyuso zao.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 “Msiharibu nchi, wala bahari, wala miti, mpaka tutakapokwisha wapiga mhuri watumishi wa Mungu wetu katika paji la uso.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

3 “Msiharibu nchi, wala bahari, wala miti, mpaka tutakapokwisha wapiga mhuri watumishi wa Mungu wetu katika paji la uso.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 “Msiharibu nchi, wala bahari, wala miti, mpaka tutakapokwisha wapiga mhuri watumishi wa Mungu wetu katika paji la uso.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 “Msiidhuru nchi wala bahari, wala miti, hadi tuwe tumetia muhuri kwenye paji za nyuso za watumishi wa Mungu wetu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

3 “Msiidhuru nchi wala bahari, wala miti, hadi tuwe tumetia muhuri kwenye vipaji vya nyuso za watumishi wa Mungu wetu.”

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

3 akisema, Msiidhuru nchi, wala bahari, wala miti, hadi tutakapokwisha kuwatia mhuri watumishi wa Mungu wetu juu ya vipaji vya nyuso zao.

Tazama sura Nakili




Ufunuo 7:3
31 Marejeleo ya Msalaba  

Na ile damu itakuwa ishara kwenu katika zile nyumba mtakazokuwamo; nami nitakapoiona ile damu, nitapita juu yenu, lisiwapate pigo lolote likawaharibu, nitakapoipiga nchi ya Misri.


Kwa kuwa BWANA atapita ili awapige hao Wamisri; na hapo atakapoiona hiyo damu katika kizingiti cha juu, na katika ile miimo miwili, BWANA atapita juu ya mlango, wala hatamwacha mharibifu aingie nyumbani mwenu kuwapiga ninyi.


Umemwadhibu kwa kiasi, ulipomfukuza; ukampepeta kwa upepo mkali katika siku ya upepo wa mashariki.


Kila silaha itengenezwayo juu yako haitafanikiwa, na kila ulimi utakaoinuka juu yako katika hukumu utauhukumu kuwa mkosa. Huu ndio urithi wa watumishi wa BWANA, na haki yao inayotoka kwangu mimi, asema BWANA.


Na ijapokuwa imebaki sehemu moja katika sehemu kumi ndani yake, italiwa hii nayo; kama mvinje na kama mwaloni, ambao shina lake limebaki, ingawa imekatwa; kadhalika mbegu takatifu ndiyo shina lake.


BWANA asema hivi, Kama vile divai mpya ipatikanavyo katika kichala, na mtu mmoja husema, Usikiharibu kwa maana mna baraka ndani yake; ndivyo nitakavyotenda kwa ajili ya watumishi wangu, ili nisiwaharibu wote.


BWANA akamwambia, Pita kati ya mji, kati ya Yerusalemu, ukatie alama katika vipaji vya nyuso vya watu wanaopiga kite na kulia kwa sababu ya machukizo yote yanayofanyika kati yake.


Waueni kabisa, wazee, na viijana, na wasichana, na watoto wachanga, na wanawake; lakini msimkaribie mtu yeyote mwenye hiyo alama; tena anzeni katika patakatifu pangu. Basi, wakaanza kwa wazee waliokuwa mbele ya nyumba.


Kama ni hivyo, Mungu wetu tunayemtumikia aweza kutuokoa na tanuri liwakalo moto; naye atatuokoa mkononi mwako, Ee mfalme.


Kisha Nebukadneza akaukaribia mlango wa lile tanuri lililokuwa linawaka moto. Akanena, akasema, Enyi Shadraka, na Meshaki, na Abednego, watumishi wa Mungu Aliye Juu, tokeni, mje huku. Ndipo Shadraka, na Meshaki, na Abednego, wakatoka katika ule moto.


Basi mfalme akatoa amri, nao wakamleta Danieli, wakamtupa katika tundu la simba. Mfalme akanena, akamwambia Danieli, Mungu wako unayemtumikia daima, yeye atakuponya.


Mtafuteni BWANA, enyi nyote mlio wanyenyekevu wa dunia, ninyi mliozitenda hukumu zake; itafuteni haki, utafuteni unyenyekevu; huenda mtafichwa katika siku ya hasira ya BWANA.


Ndipo mtakaporudi, nanyi mtapambanua kati ya wenye haki na waovu, kati ya yeye amtumikiaye Mungu na yeye asiyemtumikia.


Na kama siku hizo zisingalifupishwa, asingeokoka mtu yeyote; lakini kwa ajili ya wateule siku hizo zitafupishwa.


Naye atawatuma malaika wake pamoja na sauti kuu ya parapanda, nao watawakusanya wateule wake toka pepo nne, toka mwisho huu wa mbingu mpaka mwisho huu.


Mtu akinitumikia, na anifuate; nami nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo. Tena mtu akinitumikia, Baba atamheshimu.


Yeye aliyeukubali ushuhuda wake ametia mhuri ya kwamba Mungu ni kweli.


Lakini sasa mkiisha kuwekwa huru, na kuwa mbali na dhambi, na kufanywa watumwa wa Mungu, mnayo faida yenu, ndiyo kutakaswa, na mwisho wake ni uzima wa milele.


Naye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kulia, au katika vipaji vya nyuso zao;


tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa awe na chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya herufi za jina lake.


Kisha nikaona, na tazama, huyo Mwana-kondoo amesimama juu ya mlima Sayuni, na watu elfu mia moja na arubaini na nne pamoja naye, wenye jina lake na jina la Baba yake limeandikwa katika vipaji vya nyuso zao.


Na mwingine, malaika wa tatu, akawafuata, akisema kwa sauti kuu, Mtu awaye yote akimsujudu huyo mnyama na sanamu yake, na kuipokea chapa katika kipaji cha uso wake, au katika mkono wake,


kwa kuwa hukumu zake ni za kweli na haki; maana amemhukumu yule kahaba mkuu aliyeiharibu nchi kwa uasherati wake, na kuipatiliza damu ya watumwa wake mkononi mwake.


Kisha nikaona viti vya enzi, wakaketi juu yake, nao wakapewa mamlaka ya kutoa hukumu; nami nikaona roho zao waliokatwa vichwa kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu, na kwa ajili ya neno la Mungu, na hao wasiomsujudia yule mnyama, wala sanamu yake, wala kuipokea ile chapa katika vipaji vya nyuso zao, wala katika mikono yao; nao wakawa hai, wakatawala pamoja na Kristo miaka elfu.


nao watamwona uso wake, na jina lake litakuwa katika vipaji vya nyuso zao.


Nikasikia kama sauti katikati ya hao wenye uhai wanne, ikisema, Kibaba cha ngano kwa nusu rupia, na vibaba vitatu vya shayiri kwa nusu rupia, wala usiyadhuru mafuta wala divai.


Baada ya hayo nikaona malaika wanne wamesimama katika pembe nne za nchi, wakizizuia pepo nne za nchi, upepo usivume juu ya nchi, wala juu ya bahari, wala juu ya mti wowote.


Nikaona malaika mwingine, akipanda kutoka maawio ya jua, akiwa na mhuri wa Mungu aliye hai; akawaita kwa sauti kuu wale malaika wanne waliopewa kuidhuru nchi na bahari,


Wakaambiwa wasiyadhuru majani ya nchi, wala kitu chochote kilicho kibichi, wala mti wowote, ila wale watu wasio na mhuri wa Mungu katika vipaji vya nyuso zao.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo