Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Ufunuo 1:15 - Swahili Revised Union Version

15 na miguu yake kama shaba iliyosuguliwa sana, kana kwamba imesafishwa katika tanuri; na sauti yake kama sauti ya maji mengi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

15 miguu yake kama shaba iliyong'arishwa iliyosafishwa katika tanuri ya moto, na sauti yake ilikuwa kama sauti ya poromoko la maji.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

15 miguu yake kama shaba iliyong'arishwa iliyosafishwa katika tanuri ya moto, na sauti yake ilikuwa kama sauti ya poromoko la maji.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

15 miguu yake kama shaba iliyong'arishwa iliyosafishwa katika tanuri ya moto, na sauti yake ilikuwa kama sauti ya poromoko la maji.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

15 Nyayo zake zilikuwa kama shaba inayong’aa katika tanuru la moto, nayo sauti yake ilikuwa kama mngurumo wa maji mengi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

15 Nyayo zake zilikuwa kama shaba inayong’aa, katika tanuru ya moto, nayo sauti yake ilikuwa kama mugurumo ya maji mengi.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

15 na miguu yake kama shaba iliyosuguliwa sana, kana kwamba imesafishwa katika tanuri; na sauti yake kama sauti ya maji mengi.

Tazama sura Nakili




Ufunuo 1:15
11 Marejeleo ya Msalaba  

Kupita sauti ya maji mengi, maji makuu, Kupita mawimbi ya bahari yaumkayo, BWANA Aliye Juu ndiye mwenye ukuu.


Mataifa wananguruma kama ngurumo ya maji mengi; Lakini atawakemea, nao watakimbia mbali sana, Watafukuzwa kama makapi milimani mbele ya upepo, Na kama mavumbi vuruvuru mbele ya tufani.


Nao walipokwenda nilisikia mshindo wa mabawa yao, kama mshindo wa maji makuu, kama sauti yake Mwenyezi, mshindo wa mvumo, kama mshindo wa jeshi; hapo waliposimama walishusha mabawa yao.


Na miguu yao ilikuwa miguu iliyonyoka; na nyayo za miguu yao zilikuwa kama nyayo za miguu ya ndama; zikimetameta kama rangi ya shaba iliyosuguliwa sana.


Akanileta huko, na tazama, alikuwapo mtu, ambaye kuonekana kwake kulikuwa kama kuonekana kwa shaba, naye alikuwa na uzi wa kitani mkononi mwake, na mwanzi wa kupimia; akasimama karibu na lango.


na tazama, huo utukufu wa Mungu wa Israeli ulitokea kwa njia ya mashariki; na sauti yake ilikuwa kama mshindo wa maji mengi, nayo nchi iling'aa kwa utukufu wake.


mwili wake pia ulikuwa kama zabarajadi safi, na uso wake mfano wa umeme, na macho yake kama taa za moto, na mikono yake na miguu yake rangi yake kama shaba iliyosuguliwa sana, na sauti ya maneno yake kama sauti ya umati wa watu.


Kisha nikaona malaika mwingine mwenye nguvu akishuka kutoka mbinguni, amevikwa wingu; na upinde wa mvua juu ya kichwa chake; na uso wake ulikuwa kama jua, na miguu yake kama nguzo za moto.


Nami nikasikia sauti kutoka mbinguni, kama sauti ya maji mengi, na kama sauti ya radi kuu. Na hiyo sauti niliyoisikia ilikuwa kama sauti ya wapiga vinubi, wakivipiga vinubi vyao;


Nikasikia sauti kama sauti ya makutano mengi, na kama sauti ya maji mengi, na kama sauti ya radi yenye nguvu, ikisema, Haleluya; kwa kuwa Bwana Mungu wetu, Mwenyezi, amemiliki.


Na kwa malaika wa kanisa lililoko Thiatira andika; Haya ndiyo anenayo Mwana wa Mungu, yeye aliye na macho yake kama muali wa moto, na miguu yake mfano wa shaba iliyosuguliwa sana.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo