Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Tito 3:12 - Swahili Revised Union Version

12 Wakati nitakapomtuma Artema kwako au Tikiko, jitahidi uwezavyo kujiunga nami katika Nikopoli; kwa kuwa nimekusudia kukaa huku wakati wa baridi.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

12 Baada ya kumtuma kwako Artema au Tukiko, fanya bidii kuja Nikopoli unione, maana nimeamua kukaa huko wakati wa majira ya baridi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

12 Baada ya kumtuma kwako Artema au Tukiko, fanya bidii kuja Nikopoli unione, maana nimeamua kukaa huko wakati wa majira ya baridi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

12 Baada ya kumtuma kwako Artema au Tukiko, fanya bidii kuja Nikopoli unione, maana nimeamua kukaa huko wakati wa majira ya baridi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

12 Mara nitakapomtuma Artema au Tikiko kwako, jitahidi kuja unione huko Nikopoli, kwa sababu nimeamua kukaa huko wakati wa majira ya baridi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

12 Mara nitakapomtuma Artema au Tikiko kwako, jitahidi kuja unione huko Nikopoli, kwa sababu nimeamua kukaa huko wakati wa majira ya baridi.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

12 Wakati nitakapomtuma Artema kwako au Tikiko, jitahidi uwezavyo kujiunga nami katika Nikopoli; kwa kuwa nimekusudia kukaa huku wakati wa baridi.

Tazama sura Nakili

Tito 3:12
8 Marejeleo ya Msalaba  

Watu hawa wakafuatana naye, Sopatro Mberea, mwana wa Piro, na Aristarko na Sekundo, watu wa Thesalonike; na Gayo mtu wa Derbe, na Timotheo; na Tikiko na Trofimo watu wa Asia.

Labda nitakaa kwenu; naam, labda wakati wote wa baridi, mpate kunisafirisha kokote nitakakokwenda.

Basi ili nanyi pia mpate kuzijua habari zangu, ni hali gani, Tikiko, ndugu mpendwa, mhudumu mwaminifu katika Bwana, atawajulisheni mambo yote;

Tikiko, ndugu mpendwa, mtumishi mwaminifu, mwenzi wangu katika Bwana, atawaarifu mambo yangu yote;

Lakini Tikiko nilimtuma Efeso.

Jitahidi uwezavyo kuja kabla ya majira ya baridi. Eubulo akusalimu, na Pude, na Lino, na Klaudia, na ndugu wote pia.

Jitahidi uwezavyo kuja kwangu upesi.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo